Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

PICHA ZA MECHI: MADRID YAPIGWA 3G NA BARCELONA EL CLASICO


FC Barcelona imezidi kujichimbia kileleni mwa La Liga Baada ya kuitwanga Real Madrid kwa mabao 3-0 katika El Clasico mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Santiago Bernabeu jijini Madrid.


Kipindi cha pili kilikuwa kichungu kwa Madrid ambayo ilikubali mabao mawili ya Luis Suarez na Lionel Messi aliyefunga Kwa Mkwaju wa penalti huku Madrid ikicheza pungufu baada yabeki wake wa kulia, Dani Carvajal kulambwa kadi nyekundu baada ya kuunawa mpira makusudi akiuzuia usitinge wavuni.Alex Vidal aliyeingia dakika tatu kabla mpira kwisha, alifumga bao la tatu katika dakika ya 90 kwa mkwaju mkali kabisa, kipa alijaribu kudaka lakini ukamshinda.
Madrid walipata zaidi ya nafasi tatu za kufunga katika kipindi cha kwanza, lakini mabingwa hao wa dunia mara mbili mfululizo, walishindwa kufunga kupitia Cristiano Ronaldo na Karim Benzema.

USISAHAU KULIKE PAGE YETU HAPA


This post first appeared on Tanzania Hot News, please read the originial post: here

Share the post

PICHA ZA MECHI: MADRID YAPIGWA 3G NA BARCELONA EL CLASICO

×

Subscribe to Tanzania Hot News

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×