Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mawaziri wa Afrika Mashariki kukutana Nairobi kujadili suala la wakimbizi wa Somalia



Mawaziri kutoka nchi wanachama wa Shirika la maendeleo la kiserikali la Afrika Mashariki IGAD watakutana Alhamisi mjini Nairobi, kujadili suala la wakimbizi milioni moja wa Somalia waliokimbia machafuko yaliyodumu kwa karibu miongo mitatu.

Mawaziri hao wataapitia maendeleo yaliyopatikana katika kutekeleza Azimio la Nairobi na Mpango wa utekelezaji wa kuhudumia wakimbizi wa Somalia na kuwarudisha kwenye jamii wakimbizi waliorudi Somalia.

Shirika hilo limesema mawaziri hao wanatarajiwa kuamua hatua muhimu za kutekeleza Azimio la Nairobi na mpango wa utekelezaji uliowekwa mwaka jana, na kuhakikisha ahadi za kiufundi na za kifedha kutoka kwa wadau wa maendeleo.
Credit: China Kimataifa


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Mawaziri wa Afrika Mashariki kukutana Nairobi kujadili suala la wakimbizi wa Somalia

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×