Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Kikwete kuzindua kituo cha umeme wa gesi

RAIS Jakaya Kikwete leo anatarajiwa Kuzindua Kituo Cha kuzalishia umeme wa gesi jijini Dar es Salaam.

Kituo hicho kinachomilikiwa na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kimejengwa kwa ufadhili wa serikali kwa kutumia kampuni ya M/s Lahmeyer International ya Ujerumani ikisaidiwa na kampuni ya M/s Watsila Oy ya Finland kwa ushauri.

Kwa mujibu wa meneja uhusiano wa Tanesco, Badra Masoud, kituo kilianza kujengwa rasmi Septemba 21, 2006 baada ya kusainiwa kwa mkataba kati ya shiria hilo na Watsila ya Finland Juni 20 2006.

Alifafanua kuwa ujenzi wa mradi huu ulitumia Euro 60,272,250,00 ambazo ni sawa na Sh 99,450,000,000.00 za Kitanzania na kwamba mradi huo ulihusisha uhandisi sanifu, kuleta na kufunga mitambo itumiayo gesi kuzalisha umeme.

Alisema kituo hicho chenye mashine 12 za kuzalisha umeme aina ya 20v 34Sg kutoka Finland ambazo kila mashine moja ina uwezo wa kuzalisha megawati 8.75. Ujenzi wake ulikamilika Septemba 24 2007 na kufanyiwa majaribio Julai 30 mwaka huu.

Masoud alisema kituo hicho kinazalisha megawati 103 za umeme na kuingiza kwenye gridi ya taifa ambazo ni sawa na asilimia 15 hadi 20 za umeme wote unaosambazwa hapa nchini.

Source: Mwananchi, Nov 4, 2008



This post first appeared on Godfreyenergy, please read the originial post: here

Share the post

Kikwete kuzindua kituo cha umeme wa gesi

×

Subscribe to Godfreyenergy

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×