Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Upepo Waleta Madhara Kusini Unguja



UPOPO mkubwa ulioambatana na mvua, umesababisha Baadhi ya wananchi wa mkoa wa Kusini Unguja, kuyaacha makaazi yao baada ya nyumba zao kuezuliwa mapaa huku baadhi ya mazao yakiharibiwa.

Akizungumza na gazeti hili, Kamanda wa polisi mkoa huo, Makarani Khamisi Ahmed, alisema upepo huo ulivuna usiku wa kuamkia jana na kusababisha hasara kubwa.

Alisema nyumba zaidi ya 30 za Paje, Bwejuu na Michamvi zimeizuka mapaa na baadhi ya mabanda ya skuli ya Peje nayo pia yamezuka mapaa.

Maeneo mengine yaliyoathiriwa ni Uroa, Jambiani na Makunduchi.

Kamanda huyo alisema pia gari mbili zimeharibika baada ya kuangkiwa na mti.

“Hadi hivi sasa hakuna tukio la kufariki kwa watu lakini kuna matukio ya kupotea kwa mali za wananchi ikiwemo kuezuka nyumba mapaa na gari kuangukiwa na miti,” alisema.

Akizungumzia miundombinu ya usafiri, alisema gari zote zinazoenda maeneo ya Jumbi, Tunguu na kuendelea zimezuiliwa kupita njia ya Kibondemzungu kutokana na eneo hilo kujaa maji.

Zanzibarleo


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Upepo Waleta Madhara Kusini Unguja

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×