Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

"Viongozi CCM jishusheni kwa wananchi" Mama Samia




MJUMBE wa kamati kuu ya CCM, ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewataka viongozi kuwa karibu na Wananchi na kuacha kukaa maofisini, ili kuzijua changamoto zinazowakabili na kuzifanyia kazi.

Aliyasema hayo alipowatembelea wakulima wa bonde la Kizimbani wanaojishughulisha na upandaji wa mpunga, ikiwa ni siku ya kwanza ya ziara yake ya siku nne ya kichama, ambayo itamuwezesha kutembelea miradi ya chama kwa mikoa ya Unguja.

Samia alisema ikiwa viongozi watashuka kwa wananchi, bila shaka wataweza kutekeleza kauli mbiu ya chama kuwa CCM mpya, Tanzania mpya.

Alibainisha kuwa chama ni wananchi, hivyo ni vyema kurudi kwa wananchi, kwani awali walipotezewa matumaini, lakini wanapokwenda mara kwa mara matumaini yao watayarejesha kwa asilia kubwa.

“Kuweni na wananchi mara kwa mara na kuwazungukia kwani uongozi sio kukaa kwenye viti, bali ni kuzunguka na kujua wananchi wahahitaji nini ili muweze kuwasaidia,”alisema.

Hata hivyo, alikipingeza chama kwa kuandaa utaratibu wa kuwatembelea wananchi katika maeneo mbalimbali hasa mabondeni kwani awali ziara hizo zilikuwa hazifanyiki hivyo, kitendo hicho kinaonesha dhahiri kuwa chama kinarudi kwa wananchi.

Hivyo, alitumia muda huo kuwataka viongozi wa mkoa na wilaya kuendelea na utaratibu huo wa kuwafatilia wanyonge na kuweza kuwasaidia hatua kwa hatua.

Mbali na hayo, alisema ilani inayotekelezwa ni ya Chama cha Mapinduzi na viongozi hao ndio wasimamizi wa ilani yao kuhakikisha wanaisimamia serikali na kuona wanaitekeleza kwa kiasi gani.

Katika hatua nyengine, mjumbe Samia, alipongezwa na umoja unaoimarishwa na wananchi katika kuungana pamoja na kuijenga CCM mpya ambayo ndio inayotakiwa kufikiwa.

Wakati huo huo, mjumbe huyo akizungumza na wananchama katika Tawi la CCM Fuoni Kibondeni baada ya kuweka jiwe la msingi la tawi hilo, aliwasisitiza wananchi kurudi katika asili yao ya kushirikiana kwani anaekataa asili yake ni mtumwa.

Zanzibar Leo


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

"Viongozi CCM jishusheni kwa wananchi" Mama Samia

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×