Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Rais Kikwete ameweka wazi majina ya wabunge ya bunge la katibaHatimaye Rais Jakaya Kikwete amekamilisha uteuzi wa majina ya Wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba, litakaloanza vikao vyake Februari 18 mjini Dodoma.
Kupitia uteuzi huo amewarejesha bungeni wanasiasa wakongwe akiwamo Kingunge Ngombale Mwiru na Paul Kimiti na kuwakumbuka pia wanasiasa wakongwe ambao hawakuwahi kuwa wabunge.
Baadhi ya wanasiasa hao ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa Chama cha (NLD) Dk Emmanuel Makaidi na Mwenyekiti wa Chama cha Ustawi Tanzania (Chausta) James Mapalala.
Pia wamo Mwenyekiti wa Chama cha Democratic Party (DP), Mchungaji Christopher Mtikila na John Chipaka ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Tadea.
Bunge hilo litajumuisha wabunge wote 357 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, wajumbe 82 wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar pamoja na 201 waliotangazwa jana na kufanya idadi yao kuwa 640.
Akitaja majina hayo jana Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Dk Florens Turuka alisema wajumbe hao wameteuliwa kutoka katika makundi 10 ya kijamii.
Aliyataja makundi hayo na idadi ya walioteuliwa katika mabano kuwa ni Taasisi zisizo za Kiserikali (20), Taasisi za Dini (20), Vyama vya Siasa (42), Taasisi za Elimu (20), Makundi ya Walemavu (20), Vyama vya Wafanyakazi (19), Vyama vya Wafugaji (10), Vyama vya Wavuvi (10), Vyama vya Wakulima (20) na Makundi yenye Malengo yanayofanana (20).
“Taasisi 554 kutoka Tanzania Bara na 178 kutoka Zanzibar ziliwasilisha mapendekezo yao yaliyojumuisha majina 2,762 kwa upande wa Bara na upande wa Zanzibar yalihusisha watu 874,” alisema na kuongeza:
“Majina yote yalikuwa 3,636, lakini kinyume na sheria watu 118 walipendekeza wenyewe na kufanya idadi ya majina yaliyopendekezwa kuwa 3,754. Taasisi hizo zilileta majina mengi na kazi ya kuyachuja mpaka kubaki 201 ilikuwa ngumu,” alisema Turuka.
Alisema uteuzi huo umezingatia umri wa waombaji na kwamba wenye umri kuanzia miaka 22 hadi 35 wapo 35, wenye umri wa miaka 36 hadi 60 ni 145 na kuanzia miaka 65 na kuendelea wapo 21.
“Wameteuliwa kwa kuangalia umri, jinsi, uzoefu, sifa na mahali anapotoka mjumbe husika. Wanawake wapo 100 na wanaume wapo 101, wajumbe waliotokea Zanzibar ni 67 na waliotokea Tanzania Bara ni 134,” alisema.
Alisema katika kila kundi wajumbe kutoka Tanzania Bara wapo theluthi mbili na wale kutoka Zanzibar theluthi moja.
Katika kundi la Taasisi zisizokuwa za Kiserikali watu maarufu walioteuliwa ni pamoja na Paul Kimiti, ambaye amewahi kuwa Waziri wa Ajira na Maendeleo ya Vijana na Waziri wa Kilimo na Biashara, kati ya mwaka 1995 na mwaka 2000.
Mbali na Kimiti, pia yupo Kingunge, ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwamo uwaziri katika Serikali za awamu zote nne, tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere.
Kwa upande wa Taasisi za Kidini yupo Profesa Costa Mahalu, Askofu wa Dayosisi ya Kati Kanisa la Mennonite, Amos Muhagachi, Sheikh Mussa Yusuf Kundecha na Sheikh Hamid Masoud Jongo.
Vyama vya Siasa yumo Shamsa Mwangunga ambaye amewahi kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.
Majina kamili ya Wajumbe wa Bunge hilo ni :
Tanzania Bara (13)
1. Magdalena Rwebangira
2. Kingunge Ngombale Mwiru
3. Asha D. Mtwangi
4. Maria Sarungi Tsehai
5. Paul Kimiti
6. Valerie N. Msoka
7. Fortunate Moses Kabeja
8. Sixtus Raphael Mapunda
9. Elizabeth Maro Minde
10. Happiness Samson Sengi
11. Evod Herman Mmanda
12. Godfrey Simbeye
13. Mary Paul Daffa
Tanzania Zanzibar(7)
1. Idrissa Kitwana Mustafa
2. Siti Abbas Ali
3. Abdalla Abass Omar
4. Salama Aboud Talib
5. Juma Bakari Alawi
6. Salma Hamoud Said
7. Adila Hilali Vuai
Taasisi za Dini- (Wajumbe20)
Tanzania Bara(13)
1. Tamrina Manzi
2. Olive Damian Luwena
3. Shamim Khan
4. Mchungaji Ernest Kadiva
5. Sheikh Hamid Masoud Jongo
6. Askofu Donald Leo Mtetemela
7. Magdalena Songora
8. Hamisi Ally Togwa
9. Askofu Amos J. Muhagachi
10. Easter Msambazi
11. Mussa Yusuf Kundecha
12. Respa Adam Miguma
13. Profesa Costa Ricky Mahalu
Tanzania Zanzibar(7)
1. Sheikh Thabit Nouman Jongo
2. Suzana Peter Kunambi
3. Sheikh Nassoro Mohammed Ibrahimu
4. Fatma Mohammed Hassan
5. Louis Majaliwa
6. Yasmin Yusufali E. H alloo
7. Thuwein Issa Thuwein
Vyama vyote vya Siasa vyenye Usajili wa  Kudumu– (Wajumbe 42)
Tanzania Bara (28)
1. Hashim Rungwe Spunda
2. Thomas Magnus Mgoli
3. Rashid Hashim Mtuta
4. Shamsa Mwangunga
5. Yusuf S. Manyanga
6. Christopher Mtikila
7. Bertha Ng’angompata
8. Suzan Marwa
9. Dominick Abraham Lyamchai
10. Mbwana Salum Kibanda
11. Peter Kuga Mziray
12. Isaac Manjoba Cheyo
13. Dk Emmanuel John Makaidi
14. Profesa Ibrahim Lipumba
15. Modesta Kizito Ponera
16. Profesa Abdallah Safari
17. Salumu Seleman Ally
18. James Kabalo Mapalala
19. Mary Oswald Mpangala
20. Mwaka Lameck Mgimwa
21. Nancy S. Mrikaria
22. Nakazael Lukio Tenga
23. Fahmi Nasoro Dovutwa
24.Costantine Akitanda
25. Mary Moses Daudi
26. Magdalena Likwina
27. John Dustan Lifa Chipaka
28. Rashid Mohamed Ligania Rai
Tanzania Zanzibar (14)
1. Ally Omar Juma
2. Vuai Ali Vuai
3. Mwanaidi Othman Twahir
4. Jamila Abeid Saleh
5. Mwanamrisho Juma Ahmed
6. Juma Hamis Faki
7. Tatu Mabrouk Haji
8. Fat –Hiya Zahran Salum
9. Hussein Juma
10. Zeudi Mvano Abdullahi
11. Juma Ally Khatibu
12. Haji Ambar Khamis
13. Khadija Abdallah Ahmed
14. Rashid Yussuf Mchenga
Taasisi za Elimu- (Wajumbe 20)
Tanzania Bara
1. Dk Suzan Kolimba
2.Profesa Esther Mwaikambo
3. Dk Natujwa Mvungi
4. Profesa Romuald Haule
5. Dk Domitila A.R. Bashemera
6. Dk Jasmine Tiisekwa
7. Profesa Bernadeta Kilian
8. Teddy Ladislaus Patrick
9. Dk Francis Michael
10. Profesa Remmy J. Assey
11. Dk Tulia Ackson
12.Dk Ave Maria Semakafu
13. Hamza Mustafa Njozi
Tanzania Zanzibar (7)
1. Makame Omar Makame
2. Fatma Hamid Saleh
3. Dk Aley Soud Nassor
4. Layla Ali Salum
5. Dk Mwinyi Talib Haji
6. Zeyana Mohamed Haji
7. Ali Ahmed Uki
Watu Wenye Ulemavu- (Wajumbe 20)
Tanzania Bara (13)
1. Zuhura Musa Lusonge
2. Frederick Msigala
3. Amon Anastaz Mpanju
4. Bure Zahran
5. Edith Aron Dosha
6. Vincent Venance Mzena
7. Shida Salum Mohamed
8. Dk Henry Nyamubi.
9. Elias Msiba Masamaki
10. Faustina Jonathan Urassa
11. Doroth Stephano Malelela
12. John Josephat Ndumbaro
13. Ernest Njama Kimaya
Tanzania Zanzibar (7)
1. Haidar Hashim Madeweyya
2. Alli Omar Makame
3. Adil Mohammed Ali
4. Mwandawa Khamis Mohammed
5. Salim Abdalla Salim
6. Salma Haji Saadat
7. Mwantatu Mbarak Khamis
Vyama vya Wafanyakazi(Wajumbe19)
Tanzania Bara(13)
1. Honorata Chitanda
2. Dk Angelika Semike
3. Ezekiah Tom Oluoch
4. Adelgunda Michael Mgaya
5. Dotto M. Biteko
6. Mary Gaspar Makondo
7. Halfani Shabani Muhogo
8. Yusufu Omari Singo
9. Joyce Mwasha
10. Amina Mweta
11. Mbaraka Hussein Igangula
12. Aina Shadrack Massawe
13. Lucas Charles Malunde
Tanzania Zanzibar (6)
1. Khamis Mwinyi Mohamed
2. Jina Hassan Silima
3. Makame Launi Makame
4. Asmahany Juma Ali
5. Mwatoum Khamis Othman
6. Rihi Haji Ali
Vyama Vinavyowakilisha Wafugaji-(Wajumbe 10)
Tanzania Bara(7)
1. William Tate Olenasha
2. Makeresia Pawa
3. Mabagda Gesura Mwataghu
4. Doreen Maro
5. Magret Nyaga
6. Hamis Mnondwa
7. Ester Milimba Juma
Tanzania Zanzibar (3)
1. Said Abdalla Bakari
2. Mashavu Yahya
3. Zubeir Sufiani Mkanga
Vyama Vinavyowakilisha Wavuvi –(Wajumbe 10)
Tanzania Bara (7)
1. Hawa A. Mchafu
2. Rebecca Masato
3. Thomas Juma Minyaro
4. Timtoza Bagambise
5. Tedy Malulu
6. Rebecca Bugingo
7. Omary S. Husseni
Tanzania Zanzibar (3)
1. Waziri Rajab
2. Issa Ameir Suleiman
3. Mohamed Abdallah Ahmed
Vyama vya Wakulima-(Wajumbe 20)
Tanzania Bara (13)
1. Agatha Harun Senyagwa
2. Veronica Sophu
3. Shaban Suleman Muyombo
4. Catherine Gabriel Sisuti
5. Hamisi Hassani Dambaya
6. Suzy Samson Laizer
7. Dk Maselle Zingura Maziku
8. Abdallah Mashausi
9. Hadijah Milawo Kondo
10. Rehema Madusa
11. Reuben R. Matango
12. Happy Suma
13. Zainab Bakari Dihenga
Tanzania Zanzibar (7)
1. Saleh Moh’d Saleh
2. Biubwa Yahya Othman
3. Khamis Mohammed Salum
4. Khadija Nassor Abdi
5. Fatma Haji Khamis
6. Asha Makungu Othman
7. Asya Filfil Thani
Watu Wenye Malengo Yanayofanana – (Wajumbe 20)
Tanzania Bara (14)
1. Dk Christina Mnzava
2. Paulo Christian Makonda
3. Jesca Msambatavangu
4. Julius Mtatiro
5. Katherin Saruni
6. Abdallah Majura Bulembo
7. Hemedi Abdallah Panzi
8. Dk Zainab Amir Gama
9. Hassan Mohamed Wakasuvi
10. Paulynus Raymond Mtendah
11. Almasi Athuman Maige
12. Pamela Simon Massay
13. Kajubi Diocres Mukajangwa
14. Kadari Singo
Tanzania Zanzibar (6)
1. Yussuf Omar Chunda
2. Fatma Mussa Juma
3. Profesa Abdul Sheriff
4. Amina Abdulkadir Ali
5. Shaka Hamdu Shaka
6. Rehema Said Shamte


This post first appeared on Mchambuzi@habari Online, please read the originial post: here

Share the post

Rais Kikwete ameweka wazi majina ya wabunge ya bunge la katiba

×

Subscribe to Mchambuzi@habari Online

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×