Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Sheikhe Mkuu Dodoma alaani mauaji ya watu watano Bahi

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

SHEIKHE wa Mkoa wa Dodoma,Mustapha Rajabu amelaani vikali mauaji ya watu watano yaliyokea katika Kijiji Cha Zanka wilayani Bahi Mkoani Dodoma ambapo amewataka watanzania kuwa na roho za huruma pamoja na kukemea vitendo hivyo.

itakumbukwa hivi karibuni Katika Kijiji Cha Zanka yalitokea mauaji ya watu watano wa familia moja wakiwemo Baba, Mama, watoto wawili na mjukuu huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma likidai upepelezi bado unaendelea kuwabaini waliofanya tukio hilo.

Kutokana na hali hiyo, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Philip Mpango ametoa siku saba kwa Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwakamata wale wote waliohusika na tukio hilo.

Akizungumza  leo Januari 28,2022 wakati akitoa hotuba katika Swala ya Ijumaa katika msikiti wa Gadafi jijini hapa Sheikhe Rajabu amesema jambo hilo halikubaliki na jamii inatakiwa kukemea vikali ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa sahihi kwa wahusika ili waliofanya jambo hilo waweze kukamatwa.

“Waislamu tunatakiwa tuwe na huruma,binadamu anatakiwa awe na huruma,tupendane,hili lililotokea Zanka halikubaliki lazima tukemee kwa nguvu zote na wahusika,uislamu ni dini ya huruma ni dini ya kusaidiana tusaidiane katika hili,”amesema Sheikh Rajabu.

Amesema kumekuwa na changamoto ya ukosefu wa mvua hivyo dua zinahitajika zaidi huku akidai inawezekana mvua zikawa hazinyeshi kutokana na wengi kutenda matendo ambayo sio ya kumpendeza Mwenyezimungu.

The post Sheikhe Mkuu Dodoma alaani mauaji ya Watu Watano Bahi appeared first on News Africa Now.



This post first appeared on News - News Africa Now, please read the originial post: here

Share the post

Sheikhe Mkuu Dodoma alaani mauaji ya watu watano Bahi

×

Subscribe to News - News Africa Now

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×