Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Wizi wasababishia Tanesco Moro hasara ya bilioni 1/-

SHIRIKA la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema limekuwapo ongezeko la Matukio ya Wizi wa vifaa na kusababisha kupata hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.2 mkoani humu kwa mwaka 2006 hadi Januari 2008.

Akizungumza na mwandishi mjini hapa jana, Meneja wa Tanesco wa Mkoa wa Morogoro, Bengiel Msofe, alisema katika kipindi hicho vimeibwa vifaa mbalimbali na kulipatia Shirika hilo hasara hiyo kwa kipindi kilichotajwa.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, nyaya za umeme na vyuma ndivyo vilivyoongoza kwa kuibwa ambako kwa pamoja vimeliingizia shirika hilo hasara ya Sh milioni 676. Alisema katika kipindi hicho kumekuwa na matukio vya wizi wa vyuma na nyaya yaliyofikia 75 wakati matukio ya wizi wa mafuta ya transfoma ni 65.

Kwa mujibu wa Meneja huyo, wizi wa mafuta hayo umeharibu transfoma 67. Alisema kutokana na Mkoa wa Morogoro kuongoza katika matukio hayo ya uhujumu wa miundombinu ya shirika hilo limeisababishia utoaji wa huduma kwa wateja wake kuwa mgumu.

“Ili kuweza kuendelea kuboresha huduma za umeme katika mkoa tuwaomba wananchi kushirikiana na shirika kuwafichua wanaohujumu miundombinu hiyo kwa vyombo vya dola,” alisema.

Moja ya matukio makubwa yaliyotokea hivi karibuni katika kuhujumu miundombinu ya shirika hilo ni watu wasiojulikana kukata nguzo kubwa ya msongo wa Gridi ya Taifa kutoka Kidatu uliofanyika katika eneo la Msamvu na kuufanya Mkoa wa Dar es Salaam kupata upungufu wa umeme.
Source: Habari Leo



This post first appeared on Godfreyenergy, please read the originial post: here

Share the post

Wizi wasababishia Tanesco Moro hasara ya bilioni 1/-

×

Subscribe to Godfreyenergy

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×