Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Ukosefu wa umeme wasababisha hasara ya mamilion Zanzibar

SHIRIKA la Umeme Zanzibar (ZECO) limepata hasara ya mamilimioni ya shilingi kufuatia umeme mjini Zanzibar kukosekana kwa siku tano mfululizo.

Akizungumza na mwandishi wa Mwananchi jana, Meneja wa Shirika hilo, Juma Is-haq Bakari alifahamisha kuwa wateja wao wanaoishi katika eneo la Mji Mkongwe huingiza zaidi ya milioni 5 kwa siku, hivyo kukatika kwa umeme huo kulilikosesha shirika lake kiasi hicho cha fedha kila siku kwenye eneo hilo.

�Wateja wetu wa Mji Mkongwe wanaotumia mita za kulipa kabla (Luku) na hutuingizia zaidi ya milioni tano kwa siku, hivyo tumepata hasara kubwa, ukiachia mbali maeneo mengine ambayo yalikosekana umeme kwa siku zote hizo,� alisema.

Tatizo la kukatika umeme katika Mji wa Zanzibar limeelezwa kuwa linatokana na kukatika kwa nyaya za umeme zinazopita chini ya ardhi, ambapo maeneo mawili yalioathirika zaidi ambayo Mkele na Malindi.

Alisema mafundi wa shirika hilo walibaini kwamba tatizo hilo lilitokea kwenye eneo ambalo lina jalala kubwa ambapo taka hukusanywa na kuchomwa moto na kusababisha baadhi ya nyaya kuungua.

Alifahamisha kuwa awali mafundi walidhani uharibifu huo ulisababishwa na wachimbaji wa mifereji unaofanywa na mradi wa SALCON unaosimamiwa na Manispaa ya Mji wa Zanzibar ambapo katika vipimo vyao waliona michoro ya kampuni hiyo iliyotumia kuzika mabomba yake ya maji machafu.

Alisema mabomba hayo yaligonga waya za umeme na kusababisha hitilafu iliyotokea,

lakini baadae walibaini kwamba tatizo si hilo, bali ni joto la takataka zinazochomwa moto kwenye jalala hilo.

Kukosekana kwa umeme siku nne mfululizo kumewasababishia hasara kubwa wafanyabiashara wa Zanzibar kutokana na baadhi yao kufunga maduka kwa kukosa wateja na wageni kwenye baadhi ya hoteli za kitalii wakihamia mahali pengine.

Katika athari zilizopatikana katika hospitali ya Mnazi Mnazi mmoja watoto wawili walifariki dunia kutokana na kukosekana umeme katika chumba cha watoto waliozaliwa kabla ya muda.

Hata hivyo, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Zanzibar, Sultan Mohammed Mugheiry alisema hana taarifa ya kutokea tukio la aina hiyo na kwamba anajua kuwa kwenye hospitali hiyo kuna jenereta la kufua umeme.

Maeneo yaliyoathirika kutokana na kukosekana kwa umeme ni Jongombe, Mombasa, Mji Mkongwe, Chukwani, Kiembe Samaki, Migombani na Mikunguni.

Source: Mwananchi, 25/2/2008



This post first appeared on Godfreyenergy, please read the originial post: here

Share the post

Ukosefu wa umeme wasababisha hasara ya mamilion Zanzibar

×

Subscribe to Godfreyenergy

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×