Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mhasibu Adaiwa Kuuza Dawa Zake Badala Za Hospitali

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya mji wa Kahama mkoani Shinyanga, Anderson Msumba, amemsimamisha kazi Mhasibu wa hospitali hiyo, Millian Mwakasenge, kwa madai ya ubadhirifu wa mali za hospitalini na kuwauzia wagonjwa dawa Zake Binafsi Badala ya hospitalini.
Msumba aliyasema hayo jana wakati akizungumza na gazeti hili kufuatia madai ya uongozi wa hospitali hiyo kufikisha majina ya watu waliohusika kufuja fedha za mapato na kusababisha kupungua kwa mapato.
Alisema kutokana na agizo la Mkuu wa wilaya, kama Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, alifanya uchunguzi na kubaini chanzo ni Mhasibu wa hospitali hiyo, kuwauzia wagonjwa dawa zake binafsi badala ya kuuza dawa za hospitalini, kitendo ambacho kinakosesha mapato.
“Hospitali ya mji inahudumia wagonjwa wengi sana na asilimia kubwa inahudumia wagonjwa wa halmashauri tatu za Ushetu, Msalala na Kahama mjini,” alisema.
Aliliambia gazeti hili kuwa hatua aliyoichukua dhidi ya Mhasibu ni kumsimamisha kazi kwa muda kupisha uchunguzi huku akitakiwa kuandika barua ya kujieleza kutokana kwa ubadhirifu huo.
“Hospitali ya Kahama ina wastani wa kukusanya mapato ya Sh. milioni 32 kwa mwezi…Mhasibu huyo ndiyo msimamizi wa mapato, nikiri kwamba nimemwondoa hospitalini,” alisema.
Katika hatua nyingine Msumba alisema kwa sasa uchunguzi wa ubadhilifu huo unaendelea kutokana na agizo la Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu, timu yake itakapokamilisha uchunguzi, taarifa itatolewa kwa vyombo vya habari.
Akizungumzia kuhusu suala la changamoto la miundombinu linayoikabili hospitali hiyo, alisema bado kuna shida katika mfumo wa maji, umeme na vyoo hivyo halmashauri imejipanga kutatua changamoto hiyo.



This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Mhasibu Adaiwa Kuuza Dawa Zake Badala Za Hospitali

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×