Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Sekta Ya Nyama Yaingia Matatani Nchini Brazil

Tags: nyama kuwa brazil

Rais wa Brazil, Michel Temer, amezihakikishia nchi za kigeni Kuwa , kashfa iliyokumba sekta ya Nyama chini mwake, haina maana kuwa bidhaa zake si salama.
Rais Temer amewaambia mabalozi kuwa nchi yake bado imeendelea kuzalisha nyama yenye ubora, ingawa kumekuwa na shutuma kuwa viwanda vyake vikubwa vitatu vimekuwa vikiuza nyama iliyooza kwa miaka mingi.
Serikali ya Brazil ina wasiwasi kuwa Marekani, China na nchi za Umoja wa Ulaya zinaweza kupiga marufuku kuingiza nyama kutoka Brazil baada ya shutuma hizo za kushtua zilizojitokeza siku ya Ijumaa.
Polisi nchini humo walifanya ukaguzi nchi nzima na kushutumu makampuni ya ufungaji nyama JBS, BRF na makapuni mengine madogo madogo kwa kuuza nyama isiyo salama, kuku na bidhaa nyingine za nyama.
Zaidi ya wafanyakazi 30 wa serikali waliokuwa na jukumu la kukagua vitendo hivyo wanachunguzwa kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa.This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Sekta Ya Nyama Yaingia Matatani Nchini Brazil

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×