Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Lema awavaa wenzake kuhusu sheria wanazotunga

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema, (Chadema), ‘amewavaa’ wabunge wenzake kuhusu msumeno wa Sheria wanazotunga akiwakumbusha kuwa sheria za ovyo haziwalengi tu wananchi bali hata wao.
Aidha, alisema wapo viongozi wanaopenda kutunga sheria wakiwa katika majukwaa ya siasa, hatua ambayo inafanyika kinyume cha sheria.
Alisema hayo katika mikutano yake ya hadhara iliyofanyika jijini hapa hivi karibuni.
Alisema Sheria ya Kuzuia Utakatishaji wa Fedha Haramu, inamnyima dhamana mtuhumiwa bila sababu ya msingi.
Akitoa mfano wa Wakili Medium Mwalle, aliyemkuta mahabusu katika Gereza la Kisongo jijini, alisema amekaa mahabusu kwa miaka sita huku kesi ya msingi ikiwa haijaanza kusikilizwa.
Wakili Mwalle wa jijini hapa, alishtakiwa kwa kukutwa na kiasi kikubwa cha fedha katika akaunti yake akituhumiwa kwa utakatishaji chini ya sheria hiyo.
Alidai wakati nchi zingine za Jumuiya ya Afrika Mashariki, mshtakiwa wa kosa hilo hupata dhamana, hapa nchini shtaka hilo halina dhamana.
Kwa mujibu wa kifungu cha 13 cha sheria hiyo, mtu anayekutwa na hatia ya makosa ya kutakatisha fedha haramu adhabu yake ni kulipa faini isiyozidi Sh. milioni 500 na isiyopungua Sh. milioni 100 au kifungo kisichozidi miaka 10 au kupungua miaka mitano.
Alidai akiwa mahabusu, alishuhudia mtoto chini ya umri wa miaka 14 akiwa amefungwa mwaka mmoja kwa kosa ambalo angeweza kupewa adhabu mbadala.
Alisema adhabu ya kwenda jela gerezani ina lenga kumfanya aliyefungwa kujifunza maisha mema, lakini kwa hali ilivyo mtoto huyo na wengine hawatajifunza chochote jema isipokuwa ukatili na ulawiti.
Kuhusu viongozi kutunga sheria majukwaani, alitoa mfano wa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ambaye amewahi kusikika akisema mzazi ambaye binti yake (mwanafunzi) atakuwa amepewa mimba naye pia atashtakiwa kwenda jela.
“Hii sheria ni ya wapi, eti kwa mfano, (huku akiwaita vijana wawili jukwaani) mtoto wangu ni huyu wa kiume na mtoto wa Majaliwa ni huyo wa kike. Katika mishemishe zao mtoto wangu anampa ujauzito huyu mtoto wa kike wa Majaliwa. Sasa naye aende jela kwa kosa la mtoto wake,” alihoji.
Alisema siyo jambo jema kwa wabunge wanzake kutunga sheria hizo huku wakidhani zinawalenga wananchi huku akiwapinga viongozi wanaopenda kutunga sheria wakiwa majukwaani.
Alimtaka mbunge mwenzake, James ole Millya wa Simanjiro, kuungana na ambaye ni wakili kupinga sheria za ovyo ovyo zinazotungwa bungeni.
“Millya huyu ni mbunge mwenzangu, yeye ni wakili, sasa naomba tukiwa bungeni tukapinge sheria hizi mbovu,” alisema katika moja ya mkutano wa hadhara uliohudhuriwa pia na mbunge huyo.



This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Lema awavaa wenzake kuhusu sheria wanazotunga

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×