Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

‘Dogo’ Harmorapa ainunua bifu ya Diamond na Alikiba, achezea mvua ya matusi

Harmorapa ni kama amemwaga petrol kwenye moto wa gesi. Rapper huyo aliyeteka vichwa Vya Habari kwa sasa nchini ameonekana kuanza kuununua ugomvi wa Diamond na Alikiba.
Harmo kupitia mtandao wa Instagram, amemtuhumu Diamond kuwa ndio aliyeanza kumchokoza Kiba hivyo anapaswa kumuomba msamaha kupitia vyombo vya habari. Kupitia mtandao huo hitmaker huyo wa Kiboko ya Mabishoo ameandika:
Mimi harmorapa mfalme wa bongoflaver and social network kwa sasa nasema kiukweli kutoka moyoni bwana mdogo #diamondplatnumz wewe ndo ulie anza kumrushia vijembe vya dharau Fundi #alikiba sasa usitafute suluhu kirahisi rahisi wewe platnumz nenda kwenye midia piga goti Muombe msamaa #alikiba kwani mkosefu ni wewe na sio #alikiba .
#now_naitwa_harmo_simba
Matokeo ya alichokiandika si mazuri. Hadi tunaenda mtamboni, bado anachezea mvua ya matusi kutoka kwa Team Diamond.This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

‘Dogo’ Harmorapa ainunua bifu ya Diamond na Alikiba, achezea mvua ya matusi

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×