Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Azam FC Kwenda Swaziland kesho

Ofisa habari wa timu hiyo, Jaffar Idd,akizungumza na wanahabari.
KIKOSI cha wachezaji 23 cha Azam FC, kesho Jumatano kinatarajiwa kuondoka nchini kuelekea Swaziland kucheza mchezo wa marudiano dhidi ya Mbabane ya nchini humo.
Timu hizo ambazo zilipambana Jumapili iliyopita kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar na Azam kushinda kwa bao 1-0, zinarudiana Jumapili ya wiki hii kuko Swaziland ukiwa ni mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya pili.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ofisa habari wa timu hiyo, Jaffar Idd, alisema msafara huo utaongozana na viongozi wa timu pamoja na wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
“Kwanza nichukue nafasi hii kuwashukuru wale wote waliokuja kutusapoti kwenye mchezo wetu wa kwanza ambao tulishinda 1-0, licha ya siku ile mvua kunyesha, lakini mashabiki walijitolea kutushangilia mpaka tukapata matokeo yale.
“Kwa sasa tunaenda kwao kucheza mchezo wa marudiano ambapo kesho Jumatano ndio tunatarajia kuondoka tukiwa na wachezaji 23, viongozi kadhaa wa timu pamoja na wale wa TFF, lakini pia tayari kuna baadhi ya viongozi wameshatangulia kuweka mazingira mazuri ya kufikia timu,” alisema Idd.This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Azam FC Kwenda Swaziland kesho

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×