Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mfanyabiashara kizimbani kwa kukutwa na nyavu

RAIA wa India, Sheriaz Halari (56) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam akikabiliwa na mashitaka mawili ya kuhifadhi nyavu za kuvulia samaki zilizopigwa marufuku za thamani ya Sh milioni 427.7.
Halari ambaye pia ni mfanyabiashara, alifikishwa mahakamani leo mbele ya Hakimu Mkazi, Respicious Mwijage na kusomewa mashitaka na Wakili wa Serikali, Mossie Kaima na Wakili Mwandamizi wa Serikali, Nassoro Katuga.
Kaima alidai katika mashitaka ya kwanza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo kinyume na kifungu namba 17 (f) cha Sheria ya Uvuvi namba 22 ya mwaka 2003.
Amedai Februari 21 mwaka huu, maeneo ya Chamazi Msufini wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam, mshitakiwa alikutwa amehifadhi mifuko 106 yenye vipande 6,042 vya vyavu za kuvulia samaki vya ukubwa usiopungua inchi tatu za thamani ya Sh milioni 422.9 ambazo zimepigwa marufuku kutumika nchini.
Katika mashitaka ya pili, Kaima alidai kuwa Februari 21 mwaka huu, maeneo hayo ya Chamazi Msufini, Halari alikutwa amehifadhi mifuko minane yenye vipande vinane vya nyavu za beach seine net za thamani ya Sh milioni 4.98 ambazo zimepigwa marufuku kutumika nchini.
Mshitakiwa huyo alikana mashitaka na kwamba upelelezi wa shauri hilo haujakamilika hivyo upande wa mashitaka uliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Hakimu Mwijage alimtaka mshitakiwa kuwa na mdhamini mmoja mwenye barua kutoka serikali za mitaa au ofisini atakayesaini dhamana ya Sh milioni 10 na kusalimisha hati zake za kusafiria. Pia alitakiwa kuwasilisha hati ya mali ya thamani ya fedha za nyavu hizo za kuvulia samaki.
Mshitakiwa alikabidhi hati hiyo na kupatiwa dhamana. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 22 mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa.



This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Mfanyabiashara kizimbani kwa kukutwa na nyavu

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×