Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Vijana Kupata Mafunzo Kwa Vitendo Ili Kuongeza Sifa Ya Kuajiriwa Na Kujiajiri kwenye mpango wa miaka 5 ya Serikali

Naibu wazir wa kazi,vijana na watu wenye ulemavu Mh,Anthony Mavunde akizungumza na wadau Mbalimbali sekta binafsi katika mkutano uliohusisha serikali na sekta Binafsi uliozungumzia Mafunzo ya miaka mitano ya kuwapatia ujuzi wa kuajiriwa kwa wanafunzi wa vyuo vikuu. Asilimia 61 ya wanafunzi wanaomaliza elimu ya juu katika vyuo mbalimbali nchini hawana ujuzi na sifa za kuajiriwa kwenye sekta binafsi ili kukuza uchumi na kufikia kiwango cha kati . Hayo yamebainishwa leo na Naibu waziri wa kazi,vijana na ajira Anthony Mavunde wakati akizungumza na wadau wa makampuni ya sekta binafsi jijin Dar es salaam na kusema kuwa baada ya kugundua changamoto hiyo serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi wameanzisha mpango wa miaka 5 wa kuwasaidia vijana kupata mafunzo kwa vitendo ili kuongeza sifa ya kuajiriwa na kujiajiri. ''Tumeamua kuanzisha programu hiyo ili kuhakikisha wanasaidia nguvu kazi ya nchi kupata ujuzi wa kuweza kujiajiri lakini pia kuajiriwa katika makampuni mbalimbali yenye uhitaji wa wafanyakazi walio bora katika utendaji kazi" alisema Mavunde. Mheshimiwa mavunde akaongeza kuwa programu hiyo ya miaka 5 iliyoanza mwaka 2016 na kutegewa kumalizika na kufikia mwaka 2021 unatarajiwa kuwafikia watu milioni 4 ili kuwasaidia kukuza ujuzi na kufikia uchumi wa kati kwa kuwepo nguvu kazi ya juu ya asilimia 34


This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Vijana Kupata Mafunzo Kwa Vitendo Ili Kuongeza Sifa Ya Kuajiriwa Na Kujiajiri kwenye mpango wa miaka 5 ya Serikali

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×