Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

IJUE VALENTINE NA MAANA YAKE KIHISTORIA...

IJUE Valentine NA MAANA YAKE KIHISTORIA.. Siku maarufu duniani ijulikanayo kama ‘Valentine Day’ ama siku ya wapendanao ina historia ndefu inayotupeleka hadi miaka ya 270 yaani Karne ya 3. Siku hiyo ambayo husherehekewa na mamilioni ya watu karibia Dunia nzima tarehe 14 Februari ina mitizamo mbali mbali, yaani mitizamo ya kimahusiano/ kimapenzi, kimapendo na hata kiimani. Tutaangalia kwa uchache maana ya Valentine, uhusiano wake na masuala ya kiimani na kimapenzi/ upendo, nk. Enzi hizo za Dora ya Kirumi tarehe 14 Februari ilikuwa ni siku ya kusherehekea uzazi ambayo kwa kiingereza ilijulikana kama Fertility Rite iliyosherehekewa kila mwaka na vijana kwa kuongozana mitaani wakiwa katika jozi yaani pair, siku hiyo ilikuwa maarufu kwa kama 'Lupercalia', vijana walikuwa wakitemebea na kuongozana hadi katika sehemu za starehe, kwa kipindi hicho sehemu za starehe zilikuwa maeneo ya mijini ambapo michezo ya bahati nasibu ilifanyika. Matembezi ya vijana hao yalipambwa na vimbwenga vya namna yake, wanaume walitembea na vipande vya ngozi ya mbuzi aliyechinjwa katika siku hiyo, vipande hivyo ndio vilikuwa nguo zao za siku. Yaani hawakuvaa nguo yoyote ila kipande cha ngozi ya mbuzi kilicholowa damu. Kwa wanawake ilikuwa ni ya kustaajabisha zaidi, wao walisherehekea kwa kucharazwa mijeredi iliyolowa damu wakiamini ni njia ya kuongeza uwezo wao wa uzazi kwa miaka ijayo. Ikumbukwe kuwa Warumi walikuwa na imani juu ya miungu na hivyo kupitia matendo hayo waliamini kuwa ni njia ya kuongea na mungu wa mapenzi. Hivyo walichinja mbuzi kama sadaka kwa miungu pia. Huyo mungu wa mapenzi aliitwa ‘cupid’ ikiwa na maana. Cupid aliheshimika kama mungu wa mapenzi na alikuwa mmoja wapo kati ya idadi ndefu ya miungu ya Warumi kabla ya kukuwa kwa ukristo. Huyo mungu wa mapenzi yaani cupid alitambuliwa kwa alama ya motto mzuri wa kiume mwenye mabawa misili ya ndege na pembeni yake kuna moyo. Moyo uliashiria kitunza hisia tokea tamaduni za Urumi ya wapagani, Urumi ya miungu. Hii ndiyo sababu kuu kadi ama viashiria upendo huwa na rangi nyekundu. Kwanza sadaka ya mbuzi aliyechinjwa kwa mungu cupid, pili ilihusianishwa na hisia kwa alama ya moyo. Hivyo nguo, maua na kadi huwa na urembo wa reangi nyekundu, bila kusahau maua rozi mekundu (red roses) ambayo hutumika sana katika siku ya Valentine. Pia katika zama za kati za Ufaransa na Uingereza iliaminika ya kuwa ndege hukutana kimapenzi tarehe 14 Februari. Na hivyo kuongeza idadi ya viashiria upendo kwa wapendanao. Ndege nao walitumika kama ishara ya kufikisha hisia za upendo kwa wapenzi ama ndugu wa jirani (wapendwa). Kuna uhusiano gani kati ya Lupercalia na masuala ya kiimani?, baada ya kuingia kwa ukristo Bara la Ulaya siku za miungu nyingi zilifanyiwa mbadala na aidha mapadre mashahidi wa awali ama zilihusianishwa na maandiko matakatifu. Sherehe ya Lupercalia ikiwa mojawapo. Ni mwishoni mwa karne ya tano, yaani mwaka 496 ndipo kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki, Papa Gelasius alipotangaza mbadala wa Lupercalia kuwa siku ya kuadhimisha kumbukumbu ya mtakatifu Valetino, yaani Valentine. Inasemekana aliyeaminika kama Mtakatifu, yani Mtakatifu Valentine alikuwa ni mmojawapo kati ya mashahidi wa awali walikuwa, alikuwa ni padre na daktari. Ni chini ya uongozi wa Mtawala Claudius II Gothicus Valentino aliuawa na kuzikwa Via Flamina huko Roma. Licha ya sherehe hiyo kubadilishwa jina na lengo bado ilibakia kuwa ni siku mahususi ya kuonyesha upendo kwa wapendanao. Ilibaki kuwa siku wa wachumba kuvalishana pete na kufurahia mahusiano yao. Imebaki kuwa siku rasmi ambayo upendo unaonyeshwa kwa ishara mbalimbali kwa namna yoyote ya furaha kwa wapenzi. Siku ya mtakatifu Valentino ilianza rasmi kusherehekewa kama siku ya watu kuonyesha hisia zao za kimapenzi mnamo karne ya kumi na nne (14th C). Ujumbe rasmi ulianza kutumika karne ya kumi na sita (16th C). Marekani ilikuwa ya kwanza kutengeneza na kuuzwa kadi zikiwa na jumbe za kimapenzi karne ya kumi na saba (17th C). Miaka ya 1800 sherehe za Valentine zilikuwa maarufu sana Bara la Ulaya na Marekani na baadae kufika hadi bara la Afrika ambapo ilipokelewa ikiwa imebeba maudhui yanayofanana. Ikiwa ni siku muhimu kwa wapendanao Duniai basi imeshika upili ikifuatia kwa ukubwa baada ya sherehe za Krismasi. Ni siku kubwa ya pili kwa kupeana kadi, matembezi na ishara zote za upendo. Hadi sasa neno valentine linatumika kuonyesha upendo ama nimpendaye. Mfano, my valentine. Kwa kifupi hii ndiyo historia ya Valentine Day. Si vyema kujihusisha na jambo ambalo hujui chimbuko lake..



This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

IJUE VALENTINE NA MAANA YAKE KIHISTORIA...

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×