Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

SHINIKIZO JUU LA DAMU NA MTINDO WA MAISHA


Shinikizo juu la Damu ni ugonjwa wa kawaida ambao unaozidi kuongezeka kufuatia mabadiliko ya kuiga mtindo wa maisha wa nchi za magharibi.  Kutokea kwake kunaongezeka kulingana na umri na unajitokeza kwa zaidi kwa watu wenye umri mkubwa.  Shinikizo juu la damu husababisha athari kubwa katika moyo, figo, mfumo wa neva na macho.  Habari njema ni kwamba athari hizo zinaweza kuzuilika kwa uchunguzi na tiba ya mapema.  Mtindo wa maisha unachangia katika kusababisha ugonjwa huu na mabadiliko yake muhimu sana ili kupunguza athari zake.

Bainisho

Shinikizo la damu ni kipimo cha msukumo ambao damu huuweka kwa kuta za mishipa ya ateri wakati inapokuwa ikipita katika mishipa hiyo.  Shinikizo la damu ni matokeo ya msukumo wa damu na ukinzani wa mishipa ya damu.  Kadiri mshipa wa ateri unavyokuwa finyu ndivyo shinikizo la damu litakavyokuwa la juu zaidi.


Shinikizo la damu

Damu inasukumwa mwilini na moyo ikiwa imebeba hewa ya oksijeni na virutubisho.  Kama matokeo ya tendo la moyo la kusukuma damu na ukubwa na uwezo wa unepaji wa mishipa ya ateri inayobeba damu, damu inakuwa katika shinikizo.  Shinikizo hili la damu ni la muhimu na ni sehemu ya kawaida ya namna mwili unavyofanya kazi.

Shinikizo juu la damu linatokea wakati:

·         Mishipa mikubwa ya ateri inapoteza hali yake ya unepaji wa kuta zake.  Kwa kawaida wakati damu inaposukumwa kuta za ateri zina uwezo wa kunepa na kuruhusu upitaji, hali ambayo hupotea katika shinikizo juu la damu.

·         Mishipa ya damu inapokuwa myembamba.

Kupima Shinikizo la Damu

Shinikizo la damu linapimwa na chombo kinachoitwa, “Sphygmomanometer.”

Sijafu inawekwa kuzunguka sehemu ya juu ya mkono na kutiwa pumzi mpaka kiwango fulani halafu pumzi hiyo hupunguzwa taratibu.  Sauti ya kwanza ni sawa na sistoli, wakati sauti inapopungua inakuwa ni shinikizo la diastoli.  Siku hizi kuna mashine za elektroniki za kupimia shinikizo la damu bila ya kutumia kifaa cha kusikiliza sauti kutoka viungo mbalimbali vya mwili.

Matokeo huandikwa kama namba mbili, kama vile 120/80 mmHg (mia ishirini kwa themanini ya milimita za zebaki).

·         Shinikizo la damu la sistoli (namba ya juu) ni kipimo cha shinikizo wakati misuli ya moyo inapokaza na kusukuma damu.  Hii ndiyo kiwango cha juu cha shinikizo katika mfumo wa damu.

·         Shinikizo la damu la diastoli (namba ndogo) ni shinikizo kati ya mapigo ya moyo wakati moyo unapopumzika na kupokea damu.  Hii ndiyo kiwango cha chini cha shinikizo katika mfumo wako wa damu.

Shinikizo juu la damu linaelezewa kama shinikizo la damu la sistoli ya 140 au zaidi na shinikizo la damu la diastoli ya 85 au zaidi.  Shinikizo la damu lazima lipimwe zaidi ya mara moja katika mkao mmoja.  Kuna kile kinachoitwa shinikizo juu la damu la koti jeupe wakati shinikizo la damu lililopimwa na daktari linapokuwa juu zaidi kuliko lililopimwa na wauguzi kwa sababu ya wasiwasi.  Kwa wagonjwa wenye kisukari kiwango cha mwisho ni chini ya 130/180.  Hii ni kutokana na ongezeko la hatari ya athari za shinikizo juu la damu katika kisukari hata kunapokuwa na shinikizo chini la damu.

Watu wenye shinikizo la damu la sistoli kati ya 120 na 139 au shinikizo la damu la diastoli kati ya 80 na 89 wanachukuliwa kuwa katika hali ya kabla ya shinikizo na wanapaswa kubadilisha mtindo wa maisha kama vile lishe na mazoezi ili kuzuia magonjwa ya moyo na mishipa ya damu.

Aina za shinikizo juu la damu

Shinikizo la awali (asili)

Hii ni aina ya kawaida sana ya shinikizo juu la damu.  Hii ina maana kuwa hakuna sababu moja ya dhahiri hasa inayosababisha shinikizo hilo.

Ingawaje sababu kamili ya shinikizo juu la damu katika shinikizo la asili haijafahamika kikamilifu, inafahamika kuwa baadhi ya sababu za mtindo wa maisha zinachangia.  Ambazo ni:

1.       Ugonjwa wa figo

2.       Ugonjwa wa tezi endokrini

3.       Kusinyaa kwa aota (mshipa mkuu wa ateri)

4.       Dawa za steroidi

5.       Vidonge vya kuzuia mimba

6.       Mimba, ambayo inaweza ikasababisha dalili za kifafa cha mimba

Dalili

Watu walio na shinikizo juu la damu hawana dalili zo zote, na ndio ugonjwa huu unajulikana kama mwuaji wa kimyakimya.

Athari

Watu wenye shinikizo juu la damu wana ongezeko la uwezekano wa kupatwa na athari kubwa, ikiwa ni pamoja na:

Magonjwa ya Moyo

·         Angina pectoris (maumivu kwenye kifua wakati wa mazoezi na ambayo hupungua mtu anapopumzika.)

Hii hutokana na kusinyaa kwa mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo.  Wakati wa mazoezi mshipa huo wa ateri unakuwa hauwezi kutoa damu inayohitajika kwenye moyo.  Kwa hiyo unakosa damu ya kutosha na hivyo kusababisha maumivu ya kifua.

·         Shituko la moyo
Hili linatokea wakati kumekuwa na kuziba kabisa kwa mishipa ya ateri ya moyo na kupelekea kufa kwa misuli ya moyo.

·         Kusita kwa moyo
Hii ni hali ambapo moyo hauwezi ukasukuma damu ya kutosha kulingana na mahitaji ya mwili.  Wagonjwa hawa wanaonesha dalili za matatizo ya kupumua ambayo huzidi sana wakati wakiwa kwenye mazoezi, kuvimba miguu na wakati mwingine kukohoa.

·         Mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida.

Ubongo

·         Kiharusi
  1.      Utokaji damu – husababishwa na damu kuvujia kwenye ubongo.
  2.       Infarct – uvimbe na mlundikano wa chembe nyekundu za damu katika eneo la tishu kutokana na kuziba kwa ateri inayogawa damu katika sehemu hiyo.  Hapa hali hii kutokea kwenye ubongo na kupelekea kufa kwa sehemu husika ya ubongo.
  3.             Aina zote mbili hujitokeza na dalili za udhaifu wa ghafla wa upande mmoja wa mwili.

Figo
·         Figo kushindwa kufanya kazi ambako kunaweza kuhitaji usafishaji damu kwa mashine ya figo ubadilishwaji wa figo.

·         Dalili ni kuvimba kwa mwili, kuvimba kwa vikawa vya macho asubuhi na kupungua kwa kiwango cha utengenezaji wa mkojo.  Katika hali mbaya zaidi kunaweza kukawa na kuchanganyikiwa, mtukutiko wa mwili au degedege na ukosefu wa kutengeneza mkojo.

Macho

Hii ni kutokana na kuharibiwa na retina kutokana na mishipa midogo kwenye macho.

Mfumo wa Pembezoni wa Mishipa ya Ateri

Gangrini (kufa kwa sehemu ya mwili kutokana na sehemu hiyo kukosa mtiririko wa damu ya ateri).  Hapa kufa hutokea mikononi au miguuni kutokana na kuziba kwa ateri.

Maumivu na uchechemeaji wa vipindi vinavyosababishwa na upungufu wa mzunguko wa damu katika ateri za mguu, hali ambayo hupungua kwa kupumzika.

Ubainishaji wa ugonjwa

Kama ilivyoelezwa awali watu wengi wenye shinikizo juu la damu hawana dalili.  Wanabainishwa wakati shinikizo lao la damu linapopimwa kama sehemu ya uchunguzi wa kitabibu.

Hii ni sababu moja nzuri ya kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara na daktari wako hususani wakati una miaka zaidi ya 40.

Kurudiwa kwa uchunguzi wa shinikizo la damu kunapendekezwa ili kuhakikisha kuwa shinikizo la damu kweli liko juu.

Vipimo vya kawaida ni kubainisha sababu yo yote ya shinikizo juu la damu kama ipo, tafadhali rejea kwenye shinikizo la pili.  Uchunguzi mwingine umekusudiwa kuangalia iwapo shinikizo la juu la damu limesababisha athari katika sehemu zingine za mwili wako.

Vipimo hivyo vinajumuisha:

Uchunguzi wa mkojo wako (Protini katika mkojo wako inaweza kuwa ishara ya kwanza ya tatizo la figo)

Kipimo cha damu ili kuangalia lehemu, kiwango cha sukari kwenye damu na hali ya figo zako.
·         Kipimo cha ECG (electrocardioprogram) ambacho hunakili mabadiliko ya umeme yanayotokea katika moyo.

Ufuatiliaji

Wafuatiliaji wa shinikizo la damu

Hali hii inapaswa kufuatiliwa mara kwa mara na wataalamu wa tiba.  Kitu cha kuzingatia sana ni kwamba hakuna uwiano kati ya kiwango cha shinikizo la damu na dalili.  Hivyo ni lazima umwone daktari wako licha ya kujisikia vizuri.  Ziko mashine ambazo mtu anaweza kutumia katika kupima shinikizo la damu akiwa nyumbani.  Tunza kumbukumbu na umwoneshe daktari wako unapokwenda kumwona.

Tiba

Shinikizo la damu lililopanda kidogo halihitaji matibabu ya hima, lakini ufuatiliaji wa kawaida ni muhimu.

Kwa shinikizo la damu lililo juu sana, kulazwa hospitalini kwa ajili ya tiba inaweza ikawa ni lazima.  Wagonjwa wengi wanatibiwa kama wagonjwa wa nje.

Mabadiliko ya Mtindo wa Maisha

Acha uvutaji
Badilisha lishe yako
  1.    Kwenda kwenye mafuta kidogo
  2.    Kwenda kwenye chumvi kidogo
  3.   Kwenda kwenye lishe inayojumuisha matunda na mboga za majani.

·         Acha pombe
·         Fanya mazoezi ya kawaida:
  •             Mazoezi yawe ya kila siku na yenye kuendelea.  Kutembea mwendo wa kilomita moja kila siku inaweza kutosha.

·         Kupunguza uzito uliozidi au kudumisha uzito unaotakiwa kwa
  •      Lishe
  •      Mazoezi
  •      Epuka unene wa utotoni

Msongo

Punguza msongo maishani mwako ili kuepuka kupanda kwa shinikizo la damu kwa vipindi – jaribu mbinu za burudani au tafakuri.

Matibabu ya Dawa:

Kama shinikizo linabakia juu, daktari wako anaweza kukuandikia moja au zaidi ya madawa haya ya kushusha shinikizo juu la damu.

Utendaji wa msingi wa dawa hizo ni kama ifuatavyo:
  • Kupanua mishipa ya damu
  • Kupunguza nguvu ya kukaza kwa moyo

Makundi Muhimu ya Dawa

ACE inhibitors au angiotensin II receptor antagonists
  •       (mfano ramipril, losartan) hizi hufanya kuta za mishipa ya damu kulegea na kupanuka.

·         Zinazozuia njia ya Calcium
  •      (mfano amlodipine, nifedipine) hizi zinasaidia kupanua mishipa ya damu

·         Diuretics (eg. Bendroflumethiazide)
  •       Hizi zinaongeza kiwango cha maji na chumvi zinazoondolewa kutoka kwenye damu yako kwa njia ya figo zako.  Hii huamsha homoni zinazoteremsha shinikizo la damu.

·         Beta-blockers (mfano atenolol)
  •       Dawa hizi zinapunguza kazi ambayo moyo wako unatakiwa kufanya kwa kupunguza kasi ya mapigo ya moyo katika nyakati zile ambapo ungepiga kwa nguvu zaidi mfano wakati wa mazoezi au wakati unajisikia msongo.

Dawa utakazoandikiwa zitategemea mambo kadhaa ikiwa ni pamoja na umri wako na mbari yako.  Inaweza kuchukua muda kupata tiba bora kwa ajili yako, ikiweka uwiano wa faida na athari zo zote zinazoweza kuwapo.

Ni muhimu sana kujitolea kumeza dawa zako kila siku kwa vile watu wengi hawana dalili za shinikizo juu la damu.

Kwa nyongeza ya dawa zilizotajwa hapo juu, dawa zingine ambazo kwa kawaida huagizwa na daktari hujumisha zile zinazoteremsha lehemu, asprin kati ya zingine kwa ajili ya magonjwa ya aina hiyo.


This post first appeared on Afya Na Kiasi, please read the originial post: here

Share the post

SHINIKIZO JUU LA DAMU NA MTINDO WA MAISHA

×

Subscribe to Afya Na Kiasi

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×