Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine pdf

DownloadMwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine(Pdf)

  • Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine
  • Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine (Summary)
  • Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine (Pdf)
  • Mwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Notes
    Mwongozo Wa Tumbo Lisiloshiba Pdf
  • Uchambuzi Wa Hadithi Tumbo Lisiloshiba
  • Notes On Tumbo Lisiloshiba


Download pdf file

Mwongozo wa Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine


Wahariri


Alifa Chokocho na Dumu Kayanda (Longhorn Publishers) Waandishi


Maria Mvati


James Kanuri


Saul S. Bichwa


Dibaji


Mwongozo huu ni matokeo ya jitihada za Maria Mvati, James Kanuri na Saul S. Bichwa. The NES wameona Kuwa ni muhimu kutayarisha mwongozo huu ili kuwasaidia walimu na wanafunzi katika kuelewa hadithi zilizosheheni humu.


Hata hivyo, inashauriwa kwamba msomaji wa mwongozo huu asome kwanza hadidhi zote kabla ya kupitia mwongozo huu. Kufanya hivyo kutatajirisha maarifa yanayopatikana katika mwongozo huu.


Mwongozo huu umetayarisha hadithi zote za Lisiloshiba na Hadithi Nyingine na kuzifanya zieleweke barabara. Kuna mifano ya maswali ili kuwapa changamoto watahiniwa wote.


Wanajopo waliotayarisha mwongozo huu wana tajiriba ya muda mrefu katika kufundisha somo


Ia Fasihi ya Kiswahili katika Shule za sekondari.


Ni matumaini yangu kuwa walimu na wanafunzi hawatachoka kuusoma mwongozo huu.


James M. Kanuri


Mkurugenzi


The National Educational Services 2017


Yaliyomo


1.1 Tumbo Lisiloshiba Said A. Mohamed 5


1.2 Mapenzi ya Kifaurongo Kenna Wasike -.15


1.3 Shogake Dadangu ana Ndevu Alifa Chokocho 26


1.4 Shibe Inatumaliza Salma Omar Hamad 34


1.5 Mame Bakari Mohammed K. Ghassany 41


1.6 Masharti ya Kisasa


1.7 Ndoto ya Mashaka


1.8 Kidege


1.9 Nizikeni Papa Hapa


1.10 Tulipokutana Tena


1.11 Mwalimu Mstaafu


1.12 Mtihani wa Maisha


1.13 Mkubwa


1.1 TUMBO LISILOSHIBA —Said A. Mohamed


Hadithi inaanza kwa taharuki kuhusu uvumi uliogeuka mnong’ono ukaeneza wasiwasi-hofu. Wasiwasi ulikuwa vibanda vitabomolewa vote. Watu wakubwa walitaka kuchukua makao ya watu ili kuendeleza ujenzi wao. Kwa Mzee Mago ndiko kituo cha kuzungumzia juu ya haki zao. Yeye huwakusanya wenzake iii wajadili juu ya haki zao za kuishi pale wanapochagua. Wanahojiana mambo juu ya:


➢  Kustahili kuishi kwa amani na furaha popote nchini mwao.


➢  Namna ya kuruka vikwazo vya sheria vilivyowekwa ili watu wadogo wasiweze kupoteza mali zao.


➢  Kushawishiana watafute wanasheria waaminifu iii kutatua (mazonge ya sheria).


Wanadai kuwa wanasheria waaminifu wameadimika —hakuna haki siku hizi.


➢  Kunasihiana na kuamshana juu ya kukubali maendeleo yanayopiga kasi nchini mwao.


➢  Maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu —mdogo kwa mkubwa, wa kike kwa wa kiume.


Mtu hawezi kukimbia ukweli, upya na usasa hutazamiwa kuleta mafanikio kwa watu wote. Mzee Mago huwaonya wauchunguze huo upya na usasa waujue jmst uhvyokaa —utaleta faida au hasara. Umaskini sio ujinga. Watu maskini wangeshauriwa wangeweza kuonyesha watakavyochangia maendeleo ya nchi yao. Watu wadogo hukasirika kwani wao hufanywa kuwa kama takataka. Hasira yao ndiyo inayowapa motisha wa kusema na kujitetea. Wakubwa walidai


kuwa jiji limejaa na halina nafasi tens, suluhisho ni kubomoa baadhi ya mitaa. Jiji limejaa hoteli, mikahawa, majumba ya Mall, maduka n k. Kwa hiyo, suluhisho la uhaba wa nafasi jijini ni kubomoa sehemu zingine. Mzee Mago aliwaleta wenzake pamoja kupigania haki za hapo Madongoporomoka —pasibomolewe.


Baadhi ya wanyonge hawa wanataka wapewe visenti vyao vichache vaondoke. Wengine wanadai, hakuna kuondoka. Wanataka vvabaki pale pale na kupigania haki zao. Kabwe alisisitiza kwa nguvu kuwa wakubwa hawataweza, kwani wanaogopa umma wa


Madongoporomoka. Bi. Suruta aliwatahadharisha kuwa wakubwa hawaogopi kitu chochote.


Wakati mjadala ukiendelea, chakula cha pale mgahawani kilikuwa tayari na kikaanza kunukia na kuwatamanisha wale waliobarizi hapo. Mara likatokea jitu kubwa na kukaa mle ndani. Jitu hilo liliamuru liletewe chakula Chote cha wateja wa Mzee Mugo. Jitu hilo lilifagia aina zote za vyakula: wali wa nazi, mchuzi, nyama ya kuchoma, kachumbari n k.


Baada ya kula vyakula vyote vya mgahawani hapo lililipa hela yote kisha likaahidi kuwa kesho tena lingekuja na liandaliwe chakula mara mbili ya kile kilicholiwa. Likawaacha kwa kitendawili kuwa, kesho kama wakiamka salama kama watafungua milango ya nyumba zao zilizosimama juu ya ardhi adhimu.


Alfajiri iliyofuata, polisi wakiwa na mirau na bunduki walikuwa wanalinda askari wa baraza la mji wakiviporomosha vibanda vyote.


Kulikuwa na mahangaiko ya wanyonge wasiwasi na hatan Mbio… Hawajui waokoe mali zao duni au nafsi zao kelele’ kwenzi vilio, malalamiko, vumbi (Uk 10).


Kumbe kile kitendawili cha jitu kilimaanisha kuwa ardhi Yao ingetwaliwa yote. Hata hivyo, wanyone wanashikilia msimamO wao kuwa fujo zisingeweza kuwaondoa katikia ardhi yao.


Baada ya wiki tatu za vurugu hilo; vibanda mshenzi Vya MadongoporomOka viliota, tena vingi kuliko vya awali.


ANWANI


  • Hadithi hii imepewa kichwa ambacho kinasadifu Yale yaliyomo. Wananchi wa


Madongoporomoka walisikia


uvumi kwamba kulikuwa na mpango wa kubomoa makao yao ili kutoa nafasi ya upanuzi wa jiji. Walijadiliana mara kwa mara wakiwa katika mkahawa mshenzi wa kiongozi wao Mzee Mago. Walijadili nini? Walitaka wapate suluhisho ili kujiauni na janga hilo, hawakuwa na makao mengine.


  • Wakiwa katika mgahawa huo wanaagiza vyakula mbalimbali. Linatokea jitu moja kubwa likatoa agizo kwamba lipewe vyakula vyote vilivyokuwa vimeandaliwa wateja wengine. Lilitishia kwamba wapende wasipende angejitwalia vyakula hivyo.


  • Jitu lilikula aina zote za vyakula na kunywa chupa kadhaa za soda. Mwishowe lililipa na kuahidi kwamba lingehitaji chakula mara mbili zaidi kesho yake. Siku iliyofuata, lile jitu litifika kuja ‘kula ardhi’ ya Madongoporomoka. Lile tumbo halishibi si chakula tu, bali rasilimali za raia kama ardhi.


  • Tumbo lisiloshiba husimamia wenye mamlaka ambao hawatosheki —wanamiliki mali nyingi lakini bado wanahitaji kumiliki kite kidogo walicho nacho wanyonge. Usasa na maendeleo yameleta ahueni kwa wananchi wachochole au yamezidisha unyanyasaji? DHAMIRA


  • Mwandishi amedhamiria kuonesha namna tabaka la juu linavyokandamiza haki za wanyonge. Tabaka hili linajilimbikizia mali na kutwaa rasilimali za wanyonge bila kushiba.


MAUDHUI


Ukatili na Dhuluma


  • Wakazi wa Madongoporomoka wanadhulumiwa ardhi yao. Tabaka la mabwanyenye wanawatoa katika ardhi you no kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata kuwalipa fidia.


yao na kuwavunjia vibanda vyao pasipo hata fidia. Unyanyasaji huu unafanyika kwa kuwa wakazi


Madongoporomoka hawana mtetezi. Haki imenunuliwa wenye nacho. Hata hawajaoneshwa mahali mbadala watakwenda.


Matabaka


  • Hadithi hii inasawiri kuwapo kwa matabaka katika jamii. Kuna tabaka la mabwanyeye na tabaka la wanyonge. Tabaka la mabwanyenye linaendesha dhuluma dhidi ya wanyonge. Katika hadithi hii jitu kubwa linaonekam likisimamia shughuli ya ubomoaji wa vibanda vya wakazi wa Madongoporomoka. Tabaka hilo la mabwanyeye linatumia vyombo vya dola kama askari wa baraza Ia mji na askari polisi katika kuwakandamiza wanyonge.


Ukosefu wa Haki


Katika jamii iliyojaa dhuluma hakuna haki. Watu wa


Madongoporomoka wanaporwa haki yao ya kumiliki ardhi


Ardhi inatwaliwa na wenye nacho. Hata wanaposhauriana kutafuta wanasheria waaminifu bado wan ashindwa kuwapata. Wanasheria wamezibwa midomo kwa fedha za mabwanyenye. Haki


za watu zinasiginwa bila uteten wowote.


Umoja na mshikamano


  • Hata hivyo nguvu ya mnyonge ni Urnoja. Wakazi waMadongoporomoka wanaapa kuwa fujo hazitasaidia lolote. 1 yao kwa sababu ya fujo.


Baada ya wiki tatu za fujo hiyo wanaungana na kurejesha


WAHUSIKA


➢    Mpenda haki na mtetezi wa haki: yeye hakupuuza ule uvumi bali alijaribu kuutafutia


suluhisho


➢    Ni mwenye bidii: shughuli ya kupigania na kuzuia mipango ya watu wakubwa sio rahisi.


Ilibidi mzee Mago ajinyime, awatafute wenzake wazungumze na kulijadili jambo hili ambalo lilikuwa nyeti sana kwao.


➢    Ni mshawishi: aliwashawishi wanyonge wenzake watafute wanasheria waaminifu ili wasaidie kufafanua vipengele vigumu vya sheria kama njia ya kuwavukisha vikwazo ili wapate suluhisho.


➢    Ni mzindushi: aliwazindua wenzake na kuwapa nasaha kuhusu maendeleo. Aliwazindua kwamba maendeleo yanahitaji mchango wa kila mtu —wa kike kwa wa kiume, wadogo kwa waku bwa n k. Aidha, aliwatahadharisha kwamba wachunguze ni maendeleo gani yatakayowanufaisha.


Kabwe


➢  Anapenda ushirikiano. Alishirikianana wanyongewenzake katika kutafuta ufumbuzi wa kunyakuliwa kwa ardhi yao.


➢  Anaamini kuwa sheria inaweza kuwa suluhisho la matatizo yao.


➢  Ni mpenda amani na haki. Alitaka watafute suluhisho linalofaa kwa watu wa


Madongoporomoka.


Bi. Suruta


➢  Ni hodari katikakutoahojakwenye mashauriano. Anawapiku wanaume wote.


Bi. Fambo


➢  Mwanamke mojawapo wa wanyonge.


➢  Ni mwelewa masuala ya unyanyasaji.


➢  Anaeleza bayana kwamba wakubwa hawajali wanyonge wakihamishwa kwenye ardhi watakwenda wapi.


Jitu Ia miraba minne


➢  Hili lilikuwa ndovu —mtu kwa ukubwa wake.


➢  Ni mkubwa wa kimo: yeye alikuwa pandikizi la jitu Alipoingia katika mgahawa mshenzi watej a wote waligutuka


➢  Ni tajiri: mavazi yake ya suti na tai yalidhihirisha kuwa ni tajiri. Aidha yeye aliendeshwa na dereva wake maalum “chauffeur” katika gari Ia Audi Q 7.


➢  Ni mlafi: alikula vyakula vyote vya wateja waliokuwePO katika mgahawa wa Mzee Mago na kurudia mara tano kabl ya kushiba. Aidha alikunywa soda nyingi sana. vyakula vyote na hata hakusaza chochote.


Tanbihi; Ikumbukwe kwamba vyakula hivyo vilikuwa vimeagizva na wateja mbali mbali.


wote wamwachie vyakula vyao walivyokuwa wameagw a – wapende wasipende.


Anahusika katika uvamizi na unyakuzi wa ardhi ya


Madongoporomoka.


Umuhimu


  • Ni ishara ya wakubwa wa mji na sehemu nyingine ambao hawatosheki na mali nyingi walizo nazo. Daima hujinyakulia mali za wanyonge ili kuzidi kujinufaisha.


Maendeleo ni mazuri lakini wakati mwingine yanazusha mtafaruku katika jamii.


Wahusika wa makundi


Askari wa baraza la mji


➢  Hawa walibomoa vibanda vya wananchi wa  Madongoporomoka.


➢  Ni watiifu wa amri za wakubwa-hawakujali vilio na malalamiko ya wanyonge.


Kikosi cha polisi:


➢  Kinalinda askari wa baraza wakati wa kubomoa vibanda madongoporopoka.


Mbinu


Taharuki.


➢  Hadithi inapoanza kuna taharuki. Huo ni uvumi gani? Unazushwa na nani kwa sababu gani? Anaposema haukuwa wa kupasuka bomu au kulipuka mzinga anaendelea kuitilia uzito taharuki hiyo.


➢  Taharuki nyingine ni ile ya jitu liloingia mkahawa mshenzi lilitokea wapi? Kwa nini liliamua kuutembelea siku hiyo. Je ziara yake ni kula tu chakula au kufanya uchunguzi?


➢  Je jitu lenye tumbo kubwa lina uhusiano gani na kubomolewa kwa vibanda? Je ni kitu gani kilifanya vibanda vingi kushamiri baada ya kubomolewa?


Taswira


➢  Kuna taswira nyingi katika kisa hiki. Kuna taswira ya jitti la miraba mine kutokana na maelezo ya lile jitu lilivaa suti nyeusi na shati jeupe. Wakati mabuldoza yalipokuwa yakiangusha vibanda na kuwatimua watu. Ni taswira inayoangazia jinsi haki za


wanyonge zinavyofifishwa. Aidha jeshi la polisi hushadidia jambo hilo hilo la unyanyasaji wa w anyonge.


Balagha


➢  Haya ni maswali yasiyohitaji majibu, yanayomzindua mhusika.


➢  Mifano: yote hayo lakini yafae nini mbele ya nia ya kuhakikisha nafasi za biashara na malengo ya starehe ya wakubwa (Uk 10)


➢  Chupa mbili za Coca Cola zifae nini kwa jitu kuza kama hilo (Uk 8)


Mdokezo


➢  Maelezo machache ambayo hayakamiliki, yakitumiwa kuashiria jambo fulani. Lile jitu la miraba minne lilidokeza kwamba kungekuwa na tukio fulani. Kesho kama sote tutaamka salama. Kama tutafungua milango ya nyumba zetu zinazosimama juu ya ardhi hii adhimu.


Tashbihi


➢  Bweu lilipasuka kama mzinga (Uk 9)


➢  Kiti kilionekana kama cha Shule ya chekechea (uk 7)


➢  Kauli yajitu hilo ilimwinua Mzee Mago kama aliyechapwa bakora.


Kuchanganya ndimi


➢  Chauffeur (Uk ll)


➢  AudiQ7 (Uk10)


➢  Coca Cola


➢  Departmental stores, casinos (Uk 4)


Methali


  • Kuna matumizi ya methali kama kimya kingi kina mshindo


(Uk 3)


Takriri


➢  “Hawawezi, hawawezi kabisa hawawezi” (uk 5)


Mbinu rejeshi


➢  Uvumi kuhusu kubomolewa kwa vibanda ulianza halafu ukatoweka. Baadaye uvumi huo unarejelewa tena katika kibanda cha Mzee Mago.


Chuku


  • Ukubwa wa tumbo la mtu mwenye miraba mine limetiliwa.


chuku (uk 9)Kwa nini mwandishi amefanya hivi? Jim lilivyolamba sahani zote —halikubakisha hata ishara a chembe moja ya chakula chochote alichokula (Uk 9)


Taashira


➢  Msitari wa fedha ulipasuka kutoka mbinguni hii ni ishara za matumaini, mwangaza au nuru huashiria jambo jema.


➢  Hali ya mstari huo kumulika mpaka ndani ya mioyo ya watu na wakati huo huo uso wa lile jitu lisiloshiba kuonekana


Hii ishara ina maana kuwa ndani ya nafsi za wanyonge wakiongozwa na Mzee Mago wanajua kuwa taabu zao zinatokana na wale wakubwa wasioshiba —wakiwakiJishwa najitu ndani ya Audi Q 7.


MAPENZI YA KIFAURONGO —Kena Wasike


Muhtasari


Kifauongo ni mmea ambao majani yake hujikunyata yanapoguswa.


Dennis ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu ch Kivukoni. Ndani ya nafsi yake anasononeka kwa ufukara uliomwandama yeye na familia yak-e. Umaskini unamsumbua maana hali yake na ya watoto wa matajiri ilikuwa zimeachana wazi kabisa kama mbingu na ardhi.


Kulikuwa na tofauti katika mavazi, chakula, simu na vifaa vingine kisasa. Hali ya umaskini inamfanya asielewe yale ambayo mhadhiri


Dkt Mabonga alikuwa akiwafundisha. Licha ya tatizo lake la umaskini, Dennis amekabiliwa na ugumu wa somo hili. Dkt


Mabonga aliwakatisha tamaa wanafunzi wake kutokana na shutma zake kwamba wao hawafikirii na kutafakari mambo kwa kina kama wanafunzi wapevu wa Chuo kikuu. Alipoulizwa maswali aliwakashifu kwamba hawastahili kuwa humo kwenye darasa Ia chuoni.


Kwa Dennis hili liliongeza uzani zaidi wa tatizo lake. Dennis hakuweza kuchangamana na wanachuo wakwasi. Kulikuwa na matabaka —wenye jadi kubeli wanapitajuu na wachochole wanapita chini (Uk 17). Wanafunzi wakwasi walipoona masomo yanatatiza walikuwa na fursa ya kurejea makwao na kuendeleza miradi ya wazazi wao. Kwa Dennis hili lisingewezekana. Wazazi wake walikuwa wanategemea vibarua vya kulima mashamba ya watu


Wengine. Yeye ndoto yake ilikuwa kumaliza masomo na kupata kazi ili aweze kuumaliza ukata wake na wazazi wake.


Umaskini wake ulimfanya asiwazie hata kuwa na rafiki wa kike. Penina msichana wa tabaka Ia juu anamtembelea Dennis na kutaka


Wawe marafiki. Dennis analipinga jambo hilo kutokana na tofauti zao za kitabaka; lakini Penina anang’ang’ania kuwa tofauti zao kiuchumi haziwezi kuwa kikwazo. Penina alitaka mwanaume


ambaye ni mwaminifu. Anasisitiza, “Nataka tupige vita fikra kwanlba kijana wa kitajiri hawezi kutangamana na mwenziwe


(Uk 21)


Mapenzi ya Penina aliyetoka katika familia ya wakwasi na Dennis tkara yalidumu kwa miaka miwili. Baada ya kumaliza Chuo walnshi mtaa wa watu wastani kimapato. Pamoja najitihada zoteza kutatilta kazi. Dennis hakufanikiwa. Barua zake nyingi alizotuma hazikumletea tumaini lolote.


Fursa moja aliyopata katika shirika Ia uchapishaji magazeti aliipoteza baada ya kushindwa kujibu swali la kwanza katika mahojiano.


Mapenzi ya kifaungo ya Penina yanajitokeza wazi. Anamfukun


Dennis na kumwonya kwamba nyumba yake aione paa. Alielezea majuto yake ya kusuhubiana naye na kumkanya kwamba asije akaelezea watu wengine kwamba waliwahi kupendana.


Dennis alifungasha nguo zake na kuondoka akiwa haamini. Kumbe mapenzi ya Penina yalikuwa ya kifaurongo.


ANWANI


  • Anwani ya hadithi hii ni “Mapenzi ya Kifaurongo.Kifaurongo ni mmea ambao unajikunja Pindi tu unapuguswa na hujikunjua baada ya muda mfupi. Katika hadithi hii mhusika Penina anampenda Dennis kwa kuwa alikuwa mwaminifu. Walimaliza masomo yao lakini baada ya miaka miwili, kutokana na ukosefu wa kazi mapenzi yake yalididimia na kunyauka kabisa. Hakutaka kuhusishwa tena na Dennis. Alimfukuza kama mbwa. Ahadi zake za mapenn


zikawa kama za ule mmea. Dennis alihitaji kazi na alikuwa na ari ya kufaulu usaili lakini; anaulizwa swali moja tu na ananywea na kushindwa kujibu na hivyo anarudi nyumam bila tumaini lolote.


huduma ni sawa na mmea wa kifaurongo. Anaonesha Kuwa penzi la Penina na Dennis linanyauka baada ya Dennis kukosa kazi ambayo ingcmpatia kipato cha kumhudumia mkewe.


MAUDHUI


Ndoto za maisha.


➢  Wazazi wa Dennis walifanya juu chini ili waepukane na ukata lakini uliendelea kuwaandama. Walimsomesha Dennis wakitegemea kwamba baadaye angewasaidia lakini Dennis hakufanikiwa kupata kazi. Dennis alikuwa na ndoto zake. Alitaka kufaulu vizuri-hii ndoto ilitimia. Alitarajia kupata kazi baada ya kuhitimu ndoto hii haikutimia, licha ya yeye kuandika tawasifu yake na kuituma sehcmu nyingi.


➢  Aidha, Dennis alikuwa na matarajio ya kumwoa mchumba wake Penina. Hilo halikutokea, na isitoshe waliachana kwa njia mbaya-Penina alimfukuza atoke kwake.


➢  Dennis alikuwa na ndoto ya kuwa mtangazaji wa redio. Alifanya mazoezi mengi na kujipatia ujuzi ambao watu wengi waliafiki kwamba atakuwa mtangazaji bora mno. Hata hivyo ndoto yake hiyo haikutimia.


Matabaka


  • Dennis anatoka katika familia maskini. Wazazi wake walikuwa wachochole, hawakuwa na mali yoyote. Waliiitahidi sana kutoka katika ufukwe huo haikuwezekana walimiliki majumba mengi na wengine walikuwa misururu ya mabasi na matatu ya abiria. Shakila alikuv wa tabaka la juu —mama yake alikuwa mkurugenzi tnku wa shirika la uchapishaji. Wanachuo waliotoka tabaka laju walikuwa na maisha mazuri, libasi (nguo) zao ni bora, wan; simu nzuri, tarakilishi na vitu vingine. Dennis mavazi yak, valikuwa duni, kula kwa shida na kadhalika.


  • Kulikuwa na watu walioendesha magari ya kifahari makubwa na mazuri. Wazazi wa Dennis ni wa tabaka la chini. Walifahamu kuweka majembe begani na kulima vibarua tu.


Umuhimu wa kazi.


  • Kilabinadamu lazima afanye kazi. Kazi humzatiti binadamu. Elimu hutumiwa kama kidato cha kujipatia kazi. Kazi ndiyo msingi wa maisha. Maisha hayawezi kusonga mbele kama hufanyi kazi yoyote. Kitendo cha Dennis kukosa kazi, kinamfanya aonekane kama mzigo asiye na faida yoyote kwa Penina. Penina anaamua kuachana naye na kumfukuza kabisa atoke kwake


Mapenzi


  • Wanafunzi wa Chuo cha Kivukoni wanaonekana wengi wao kuwa na mahusiano ya kimapenzi. Wale wa tabaka muia huonekana wakiongozana mvulana na msichana kufanya starehe za hapa na pale.


  • Aidha, Penina mtoto kutoka katika tabaka la wenye nacho, anasalitiwa na mpenzi wake ambaye naye ni wa tabaka la juu. Katika kutafuta suluhisho Ia mapenzi ya dhati Penina anaamua kupelcka mapenzi yake kwa Dennis ambaye anatoka katika tabaka la chini. Mapenzi yao yananoga kama kinu na mchi wakati wakiwa chasm. Penzi linakuja kuwa Ia kifaurongo pale wanapomaliza chuo na Dennis kukosa kazi


Wahusika


Dennis


➢  Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni.


➢  Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu.


➢   Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye.


➢  Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; “Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa” (Uk 20)


➢  Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni.


➢  Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.


➢  Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi.


➢   Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-“Sikomi kuyamezea mate hayo”. Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri


Kutokana na ukata wa wazazi wake, Dennis anaishi maisha ya kimaskini chuoni. Anakuwa mpweke chuoni. Umaskini wake ulimfanya asijiamini na aghalabu alikuwa mwenye huzuni. Anaisitikia hali yake duni, akawa msononevu. Anabahatika kupendwa na Penina, msichana mrembo kutoka familia ya kitajiri. Mvuto wa Penina unamfanya Dennis abadili msimamo wake wa awali-akasalitika na kukubali kuwa na mahusiano naye. Ukosefu wa ajira unamfanya afukuzwe na Penina-akajikuta mpweke tena asiye na makao. Kauli ya Dennis ya hapo awali ikatimia; “Mapenzi hukua, huugua yapatapo maradhi na hufa” (Uk 20)


Ni mvumilivu: anavumilia hali yao ya umasikini na ukosefu wa vifaa vya kisasa alipokuwa chuoni. Ana bidii: anajitahidi sana katika masomo hadi akafaulu vyema. Alisomea kijijini kwenye shule


za kawaida lakini akafaulu na kuingia chuo kikuu.


Alitafuta kazi kwa bidii, alituma tawasifu yake mahali pengi. Ana tamaa: alitamani awe na rafikimpenzi kama wanachuo wengine. Kuwa na gari la kifahari-“Sikomi kuyamezea mate hayo”. Alitamani hali njema ya siha mavazi bora ya watu wakwasi. Alitamani wazazi wake wangekuwa matajiri


Mwenye hasira: anamkashifu Dennis kwa kasbfa no kukosa kazi,


Umuhimu Wake


Ametumiwa kuangazia ugumu wa kupata apra hata ya kupata shahada. Aidha. Dennis ametumika kudhihirisha kuwa si Rihisi kijana wa kiume mchochole kupendwa na msichana wa tabaka la juu na mahusiano yao kudumu.


Penina


  • Mwanachuo wa Chuo kikuu cha Kivukoni.


  • Msichana kutoka kwenye familia yenye utajiri mwingi.


  • Baba yake Bw. Kitime ni Katibu wa kudumu katika Wizara ya Fedha.


  • Penina anapata masurufu mengi ya kutosha, shilingi elfu tano kila juma.


  • Ni mshawishi: alimshawishi Dennis kuwa pesa na mapenn ni vitu tofauti. Dennis alikubaliana naye.


  • Ana tamaa ya mapenzi: ingawa alipewa pesa za kutosha alikuwa na majonzi kwa ajili ya kukosa mpenzi.


  • Ni jasiri: alimpasulia Dennis ukweli kuwa amempenda na anataka wawe wapenzi badala ya kusubiri afuatwe yeye.


  • Hana uvumilivu sana: aliweza kukaa na Dennis kwa miaka miwili tu akamtupa nje ya nyumba yake.


  • Ni mwenye msimamo: alikata kauli ya kupendana na mwanaume asiye na pesa. Alitoa uamuzi kwamba hataolewa mpaka Dennis apate kazi kubwa. Alipokosa ajira anamfukuza na kumtukana.


  • Hana subira: aliweza kumvumilia Dennis kwa kipindi Cha miaka miwili tu-


  • Mwenye hasira: anamkashia Dennis kwa kashfa kali kutokana na kukosa kazi.


  • Mdadisi: aliweza kujua jina Ia Dennis hadi chumba chake katika Mastura Hall. Alijua kuwa Dennis hana fedha na kumweleza bayana.


Umuhimu


Anadhihirisha kuwa sio rahisi msichana wa tabaka Ia juu kuolewa na mvulana mchochole.


Dkt Mabonga


  • Mhadhiri wa Chuo kikuu.


  • Anaifahamu mada yake ya fasihi vyema.


  • Anakatisha wanafunzi tamaa kwa majibu yake ya mkato na makavu.


  • Mkweli: hasiti kusema yale yaliyomo moyoni hata kama yataleta maudhi.


  • Ingawaje ni msomi anashindwa kuwafafanulia wanafunzi wake dhana ngumu zinazowatatiza.


Umuhimu


  • Ametumiwa kudhihirisha ugumu wa masomo ya Chuo kikuu na namna walimu wanavyohitaji wanafunzi watafute maarifa wao wenyewe.


Shakila


  • Mwanachuo na mwanamji wa Kivukoni.


  • Msichana am baye hakupata shida za kutafuta kazi.


  • Ana mlahaka mwema: anamkumbuka na kumsalimia vizuri Dennis wakati Dennis ameenda kuomba kazi.


  • Ni mwenye maiivuno


  • Ni mwenye majivuno: alijigamba chuoni kwamba yake ni mkurugenzi wa shirika moja la kuchapisha


  • Ni mfariji: anampa moyo Dennis kwamba Mungu apate kazi ile.


Umuhimu


  • Kudhihirisha matabaka yaliyo katika jamii.


Bwana na Bi. Kitime


  • Hawa ni wazazi wa Penina.


  • Bwana Kitime ni Katibu wa kudumu wa Wizara ya Fedha.


  • Ni wakwasi, wako katika daraja la juu.


  • Wanamtumia binti yao fedha za kutosha kila wiki.


  • Wanampa binti yao malezi ya hali yajuu kwani wanajiweza.


  • Wanawapatia Penina na Dennis masurufu yote wakielewa fika kuwa hawana kazi.


  • Ni washauri: walimtahadharisha Penina kuhusu kuolewa na mchochole asiye na kazi.


Hata hivyo walimwachia Penina uhuru wa kujiamulia.


Mbinu


Taharuki


  • Kuna taharuki, wakati mlango wa Dennis unapogongwa: Mja huyo ni nani, Penina alijuaje kuwa huyu kijana anaitwaDennis.


  • Wakati kisa kinapomalizikia pia kuna taharuki: Je Dennis alienda wapi? Alipata mastakimu vipi bila fedha? Penina aliendelea kuishi katika nyumba ile.


Balagha


  • Wavulana wangapi wamejikuta wakining’inia bila kupenda kwao’? (Uk 18)


  • Kwani swali langu liko vipi? Kwa nini wanafunzi anacheka? Maswali haya yanamhusu


Dennis. Kwa nini ninalia sasa (Uk 13)


  • Fukara aliyefukarika mpaka mwisho aseme mm mbele ya wanaojigamba na kujishaua?(Uk 16) …


  • Nitawalipaje wazazi wangu wema walionitendea (Uk 25)


Tashbihi


  • Ninahangaika kama kondoo aliyevamiwa na jeshi la usubi (Uk 25)


  • Nimetoka ofisini kama mgonjwa mahututi.


  • Nimeweweseka kama ubua (Uk 25)


  • Mapenzi ni matamu kama uki (Uk 16) Yametengana kama ardhi na mbingu (Uk 17)


  • Njaa inanitafuna kama mbwa anavyouguguna mfupa (Uk 17)


  • Kutetemeka kama aliyenyeshewa na mvua kubwa kumwibua bingwa ni kama kupata maziwa kutoka kwa kuku (Uk 13)


Methali


  • Mzoea sahani vya kigae haviwezi (Uk 20)


  • Ujapokosa la mama hata la mbwa huanwa (Uk 17)


  • Mwana wa kuku hafunzwi kuchakura (Uk. I 5)


  • Mtu huvuna alichopanda (Uk 20)


  • Mzungu wa kula haufunzwi mwana (uk 15 )


  • Mgomba changaraweni haupandwi ukamea (Uk 27)


Misemo


  • Hazipunguzi hazizidishi (uk 21)


Utabiri


  • Dennis alitabiri vile ambavyo Penina alimpenda wakati huo” akasema kesho anaweza kuwa chanzo cha kero na usumbufu. Huba litakuwa limekufa na kufukiwa kaburini.


  • Hili lilitokea baada ya kukaa kwa miaka miwili na mchumbake Penina.


Litifai


Kuna maneno yaliyodondolewa katika riwaya ya utengano “Na nyumba hii uone ” (Uk 27)


Kuchanganya ndimi


  • Your competence is doubtful, (uk 25)


  • Tarmacking (uk 26)


Mjadala wa nafsi


  • Dennis anapofukuzwa anajizungumzia sijui kama mimi ndiye kupe au mlazadamu.


1.3 SHOGAKE DADA ANA NDEVU —Alifa Chokocho


Bwana Masudi na Bi. Hamida ni mtu na mkewe. Wamejaliwa kupat binti aitwaye Safia. Kabla ya kulala wazazi hawa huzungumz mambo mazito yanayogusa mioyo yao. Walimsifia sana binti


yao kwa vile alivyo na mwenendo mzuri. Safia ana tabia inayowafurahisha wazazi wake. Shuleni anafanya vyema kabisa. Wazazi hawa walielewa vyema kabisa kuwa kupata mtoto na kumlea ni mambo mawili tofauti “…kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza “


(Uk 29)


Walijadili ukweli kwamba wapo wazazi waliojali wa watoto, lakini wakawa balaa. Wakakosa manufaa kwa wazee wao na jamii nzima.


Bi. Hamida anatoa mfano wa mtoto wa Habiba Chechei aitwaye Mkadi. Mkadi ana vitendo viovu kushinda shetani. Walimlinganisha Mkadi na Safia na kuona binti yao ni safi hana doa.


Sifa nzuri za Safia zilienea hadi kwa marafiki na watu wote wanaoingia na kutoka kwa Bwana na


Bi. Masudi. Kwa nini anasifiwa hivyo?


  • Husaidia wazazi wake.


  • Husaidia kazi zozote habagui.


  • Yeye ni hodari sana shuleni.


  • Kila mtihani huibuka wa kwanza.


  • Humwogopa Mungu na kufuata sheria zake zote.


  • Safia hujiongoza na kufanya hayo yote bila kushurutishwa na mtu yeyote. Hayo yote aliyalifanya wazazi wake wakashukuru kupita kiasi.


Safia aliwataka wazazi wake wamruhusu Kimwana shoga yake aje ili wajitayarishe vyema kwa mtihani wa kuingia kidato cha kwanza.


Wazazi wa Safia walikubali wasemavyo wahenga kuwa, . kidole kimoja hakivunji chawa. Analolijua Safia, Kimwana halijui.


analolitambua Kimwana Safia hana habari nalo e ” (Uk 31)


Wk 30 Baada ya muda, Kimwana akaanza kuja nyumbani kwa akina Safia na wakawa wanasomea chumbani. Wakaomba kufunga mlango ili wasisumbuliwe na Lulua, ndugu mdogo wa Safia. Wazazi wao wakawaruhusu wafunge mlango kwa ndani. Baada ya muda kupita, Bi. Hamida akawa ana shaka ya kuwa Safia ni mjamzito. Akaanza kuona dalili zote —kutapika na kunyong’onyea na hana uchangamfu. Alipomdadisi, Safia alikasirika na kumlaumu mama yake. Hata hivyo Bi. Hamida alitia shaka, akachanganyikiwa-Safia anasema uongo au ukweli. Alimuuliza mumewe, ambaye alisema kuwa Safia hawezi kuwa mjamzito. Siku moja wakila chamcha, Lulua alitoboa siri kwamba, aliingia chumbani mwa Safia akawakuta wamelala. Na shogake Safia alimwona ana ndevu. Wakati huo huo Bw. Masudi akapata ujumbe kwa simu uliomgutusha —Safia aliyekwenda kliniki kutoa mimba amekufa. Bi. Hamida na Bw. Masudi wakachukue maiti.


ANWANI


➢  Anwani ya hadithi hii inasadifu yale yaliyomo. Safia binti wa Bwana Masudi na Bi.


Hamida anajulikana kuwa ana nidhamu ya hall ya juu. Ni mtiifu, anafanya kazi zote za nyumbani na shuleni anaongoza. Wazazi hawa walijua fika kuwa Mungu amewajalia. Kwa imani ya dini, Safia alikuwa mcha Mungu kabisa.


➢  Ili kujitayarisha na mtihani wake wa mwisho, Safia aliomba rafiki yake aje kwao wadurusu pamoja. Wazazi wake bila shaka wakamkubalia. Kimwana aliyeaminika kuwa na tabia kama ya Safia akawa anakuja kudurusu. Wakimaliza alirejea kwao. Kuzuia usumbufu wa Lulua ndugu mdogo wa Safia, wazazi wakawaruhusu kujifungia ndani.


➢  Safia alianza kuwa mnyonge na kutapika. Mama mtu akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, hakuafikiana  naye wakati walicheza aliwahi kujitoma chumbani akaingia shaka. Alipomshirikisha mumewe, nayc, V,ulua wakati walicheza aliwahi kujitoma chumban akawakuta Safia na shogake wamelala —na shogake ana ndevu Safia alikuwa mjamzito na katika shughuli za kutoa akafariki. Mimba ni ya shogake mwenye ndegu.


DHAMIRA


  • Mwandishi amedhamiria kuwakumbusha wazazi kuongeza umakini katika malezi ya watoto. Wasiwaamini watoto wao asihmia mia moja.


MAUDHUI Changamoto za Malezi


➢  Wazazi wanaweza kujitahidi kutoa malezi yanayofaa lakini maamuzi ya kuwa na


mwenendo bora ni juu ya mhusika mwenyewe. Mtoto wa Bi. Habiba Chechei aitwaye Mkadl alisemwa kuwa ana tabia chafu sana. Safia alionekana mwenye tabia nzuri. Na alipoamua kuwa mzuri alitekeleza majukumu yote —kusaidia kazi za nyumbani, kuheshimu watu na kutia bidii masomoni. Kwa upande mwingine aliamua kufanya mapenzi kabla ya wakati akijua kuwa sio vyema.


➢  Aidha anasema uongo kwa mama yake. Jitihada za Bi Hamida za kutaka ajue ukweli zikagonga mwamba. Safia akaarnua kutoa mimba ingawa alielewa ni kosa. Na alifariki. Akawaachia wazazi na jamii nzima mshangao na masikitiko


Unafiki na Uongo


➢  Safia alikuwa mnafiki na mwongo. Alijifanya kwamba ana tabia safi kama umande, kumbe alikuwa na tamaa ya ngono Wanakijiji wanamsema vibaya mtoto wa Hamida Chechei na kumfananisha na mbwa. Hawakumsengenya Safia kwa sababu mbele ya macho yao alikuwa na tabia nzuri. Mama anapomuuliza na kumdhihirishia kwamba anamshuku, anapandisha hasira. Baba Safia, Bw. Masudi, alimwamini binti yake mno, hata akakashifu fikra zake. Matokeo yake Safia anafikia hatua ya kudanganya kuwa yule anayesoma naye chumbani ni binti kumbe njemba yenye ndevu.


Tamaa za vijana


➢  Safia anajitahidi kwa kila jambo, masomo aliyamudu vyema. Anasifika kwa kazi za nyumbani kama vile kupika, kufua, kupiga pasi na kadhalika. Kanuni au sheria za dini alizizingatia bila wahaka (wasiwasi) wowote. Hata hivyo anawaka tamaa ya kufanya mapenzi. Anaamua kutumia ujanja kwa kutoa ombi ambalo halikuwa na shaka kwa wazazi wake. Na yeye akajichimbia kaburi mwenyewe


➢  “Kimwana” anaye anakuwa na tamaa. Alijifutika kwenye buibui na kujifanya kuwa yeye ni kimwana shoga yake Safia. Udanganyifu huo umeleta hali ya mtafaruku kwa wazazi wa Safia. Bi. Hamida anakosa furaha kabisa. Huenda njemba hii hatawahi kujulikana daima kwa kuwa muda wote ilijifutika buibui lililoficha use wake.


Umbea


➢  Bi. Hamida na wanawake wengine wa mtaani walikuwa wambea. Wamemkashifu na kumuumbua Mkadi, mtoto wa Habiba Chechei. Wanamwita kwamba yeye ni mbwa koko na uovu wake umezidi wa shetani. Bi. Hamida baada ya mtoto wake Safia kumwendea kinyume hataweza kusema lolote.


Bidii katika Kazi


➢  Kutia bidii katika shughuli yoyote zile huleta tija. Awali bidii masomo zilimpatia sifa nzuri Safia kwa sababu alikuwa wa kwanza hadi mwaka wa mwisho. Aidha bidii yake ya kazi za nyumbani, , staha yake na ucha Mungu ulitambuliwa na kila mtu.


Mikasa Maishani


➢  Bw. Masudi na Bi. Hamida walikuwa na maisha ya utulivu.Wanandoa hawa wawili walikuwa wanaelewana. Upendo na ushirikiano wao hujidhihirisha kwa vile wanavyozungumzia mambo mazito ya nafsi zao. Baada ya kufurahia mwenendo wa binti yao —furaha inakatika ghafla. Wanajikuta katika hali ya kupatwa na janga — janga la kifo cha ghafla cha mwanao na soni mbele ya macho yao.


Tabia na Mienendo ya Vijana


➢  Vijana mara nyingi huwa na mihemko ya kupapia mambo kabla ya wakati. Mkadi alikuwa na mwenendo usiofaa.Wanawake wambea akiwemo Bi. Hamida wakamsengenya.Safia naye katafuta njia ya kukidhi tamaa zake kwa njia mwafaka. Wazazi wake mwenyewe wakarahisisha mambo kwa kuwapa ruhusa ya kujifungia ndani. Sio rahisi kutambua mienendo ya vijana. Ni vyema kuviepuka vitendo viovu maana matokeo ya uovu hayafichiki. Bi. Hamida anaanza kutilia shaka unyonge wa Safia na kutapikatapika kwake. Shaka haikuwa uongo bali ukweli mtupu.


Hila na Ujanja


➢  Safia alitumia maarifa na ulaghai kuwahadaa wazazi wake. Alijua fika namna atakavyowateka akili bila hata kumtilia shaka. Ujanja wake na hila ukamwezesha kufanya mapenzi ndani ya nyumba ya wazazi wake. Dalili za mimba zilipoanza kudhihirika akasingizia homa ya malaria sugu. Alidanganya kwamba alienda hospitalini. Anapoona mama anam shuku, anatumia ujanja mwingine kuzibia hila zake- Anafanya hila za kuitoa mimba na hatimaye anaonja pepo mwenyewe.


Imani ya dini


➢  Dini ni dhana mwafaka ya kumwongoa mtu ili awe mnyofu. Hata hivyo dini inaweza kutumiwa visivyo. Safia alijifanya kwamba ni mshika dini mno —hadi wazazi wake hawakumshuku kwamba anaweza kuwaendea kinyume.


➢  Daima alijifunika ushungi hata akiwa humo ndani mwao.Anatumia mwamvuli wa dini kujificha na kufanya uovu mtupu.


MBINU


Methali


➢  Kuzaa mwana si pato, pato ni kumvyeleza (Uk 29)


➢  Lisemwapo lipo, kama halipo linakuja (Uk 30)


➢  Siri ya kata iulize mtungi (Uk 30)


➢  Kidole kimoja hakivunji chawa (uk 31)


Tashbihi


…bintiye aliye safi kama umande s


….hikamoo inayotoka nyuma ya buibui kama kata ya maji mtungini.


Mjadala wa nafsia/ uzungumzi nafsia


  • Bi. Hamida, baada ya kuona hali ya mwanae ya unyonge na kutapika.


Mdokezo


  • Kidugu kidogo cha Safia kilisimulia kisa shogaye kuwa na ndevu kwa kudokeza kidogo kidogo. Juzi… Juzi… Ivyo (Uk 34)


Taharuki


Baba Safia anapoelezwa juu ya kifo cha mwanae alishikwa na mshangao mkubwa. Hatujui vile alivyoathirika. Aidha hatujui vile mama yake Safia alivyochukulia jambo hilo.


WAHUSIKA


Safia


➢  Huyu ni binti wa Bw. Masudi na Bi. Hamida.


➢  Anasifika mno kwa tabia yake nzuri isiyokuwa na doa lolote


➢  Katika masomo yake alikuwa anaongoza darasa.


➢  Ana kipawa cha uzingativu wa kiwango chajuu.


➢  Ni msaidizi mkuu wa mama yake Bi. Hamida.


➢  Anamudu kazi zote za nyumbani.



This post first appeared on Nabiswa, please read the originial post: here

Share the post

Muhtasari Wa Tumbo Lisiloshiba Na Hadithi Nyingine pdf

×

Subscribe to Nabiswa

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×