Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Askofu Dr Getrude Rwakatale Afariki


Askofu   Dr Getrude Rwakatale  wa Kanisa la Mlima wa Moto amefariki Dunia Alfajiri  Aprili 20, 2020.Taarifa hiyo imetolewa na Mwanaye Mutta Rwakatare, wakati akizungumza na  kituo kimoja cha radio Jijini Dar es salaam.
"Ni bahati mbaya imetokea asubuhi ya leo saa 11 kasoro, alikuwa na matatizo ya moyo, jana tulimkimbiza Hospitali lakini bahati mbaya imetokea, tupo katika hatua ya kuangalia namna gani tutafanya ili tuweze kumpumzisha mama yetu" amesema Mwanae Muta Rwakatale .

Alizaliwa Disemba 31, 1950, hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 70.
Ikumbukwe kuwa Mama Rwakatare aliwahi kuwa Mbunge wa Viti Maalum wa Mvomero kuanzia mwaka 2008 hadi 2015, na baadaye mwaka 2017 aliapishwa na Spika wa Bunge Job Ndugai, kama Mbunge wa kuteuliwa na Rais wa kipindi hicho Dkt Jakaya Mrisho Kikwete.
Mazishi Ya Dr Getrude Rwakatale  Yatafanyika Jijini Dar es Salaam Katika Kanisa Lake na Msiba Utaudhuriwa na watu wachache  zaidi Kuwai kutokea kwa watu Maarufu Hii ni kutokana na janga la Corona/Covid-19.


This post first appeared on SUMBI ONLINE BUSINESS, please read the originial post: here

Share the post

Askofu Dr Getrude Rwakatale Afariki

×

Subscribe to Sumbi Online Business

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×