Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Hoja Sita Za ACT-Wazalendo kwa Humphrey Polepole


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo, Ado Shaibu ametumia hoja sita kumjibu Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM, Humphrey Polepole aliyepinga uchambuzi wa awali uliofanywa na chama chake, kuhusu ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali-CAG, Prof. Mussa Assad ya ukaguzi wa mapato na matumizi ya fedha za umma kwa mwaka 2016/17.

Ado ametoa hoja hizo leo wakati akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, ambapo amewataka Watanzania kumpuuza Polepole aliyemuita CAG wa CCM ambaye alisema masuala nane yaliyotajwa na ACT kutoka katika ripoti ya CAG kuwa ni hatari, ni ya uongo.

Akielezea baadhi ya hoja kati ya sita alizotoa leo katika kupinga madai ya CCM kwamba ACT ni chama kidogo kischokuwa na uwezo wa kufanya uchambuzi wa ripoti ya CAG, Ado amesema chama chake kimekuwa na utamaduni wa kuchambua bajeti zote kwa kutumia weledi, ujuzi na uzoefu na ndiyo sababu ya kuhofiwa na serikali pamoja na CCM.

Hoja nyingine aliyoitoa Ado, ni kwamba hakuna fedha ghafi na au tarajiwa zilizokusanywa na serikali kama alivyosema Polepole na kwamba serikali yenyewe imetoa ushahidi wa nyaraka juu ya namna fedha ambazo serikali imeshazikusanya.

Vile vile, Ado ameipinga hoja ya uwepo wa fedha za serikali ya Zanzibar kama ilivyosemwa na Polepole kwa madai kuwa kama zingekuwepo zingeripotiwa kwa kuwa serikali ilikuwa na miezi mitatu ya kuzionyesha pamoja na kupata muda wa kujadiliana na CAG kuhusu hoja alizoziibua.

“Labda tu mwenezi wa CCM haelewi ‘Hati Fungani’ ni nini. Ndio maana anaropoka tu kuwa Serikali inasubiri hati fungani zake ziive ili iweze kulipwa shilingi 697.85 bilioni zake. Kwanza Serikali ndio huuza hati fungani, watu, makampuni, mabenki, taasisi na asasi ndio hununua hati fungani, na zinapoiva hizo hati fungani, Serikali ndio hulipa amana na riba za iliowauzia hati fungani. Sasa mwenezi wa CCM hajui hata jambo hili rahisi kuhusu masuala ya kibenki?,” amehoji Ado wakati akitoa hoja za kumpinga Polepole.

“Serikali hupata sehemu kubwa ya mikopo ya ndani kwa utaratibu wa kuuza hati fungani, na hulipia hati fungani hizo (zilizoiva) kwa utaratibu wa kulipa amana na riba. CAG ameonyesha namna mikopo ya ndani ilivypatikana kupitia hati fungani, na pia amefafanua namna madeni ya riba na amana za hati fungani zilizoiva yalivyolipwa,” amesema.


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Hoja Sita Za ACT-Wazalendo kwa Humphrey Polepole

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×