Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Barbara Bush Afariki Dunia

Barbara Bush, mke wa aliyekuwa Rais wa zamani wa Marekani na Mwanaharakati Amefariki Akiwa na umri wa miaka 92.

Barbara Bush, mke wa aliyekuwa rais wa zamani wa Marekani na mwanaharakati amefariki akiwa na umri wa miaka 92.

Ndiye aliyekuwa nguzo ya kisiasa ya marais wawili wa taifa hilo akiwemo mumewe George HW Bush na mwanawe George W Bush.

Bi Bush ambaye alikuwa mke wa rais kutoka 1989 hadi 1993 amekuwa akidorora kiafya kwa muda sasa na alikuwa amekataa kupatiwa matibabu zaidi.

Risala za rambirambi zimetumwa nchini Marekani kutoka maeneo tofauti duniani.

Mumewe aliye na umri wa miaka 93 ndiye rais aliyeishi kwa muda mrefu nchini Marekani.

Barbara Bush na mumewe aliyekuwa rais wa Marekani George HW Bush

Mwana wao George alichaguliwa 2000 na kuhudumu kwa miula miwili kama rais wa 43 wa Marekani.

Katika tanzia alisema katika taarifa yake kwamba ''mamangu mpendwa ametuwacha akiwa na umri wa miaka 92. Laura Barbara, Jenna na mimi tunaomboleza , lakini roho zetu zimepumzika kwa sababu tunajua yake pia imepumzika.

BBC Swahili


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Barbara Bush Afariki Dunia

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×