Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Watu 257 wapoteza maisha katika ajali ya ndege ya kijeshi Algeria




Ndege ya kijeshi ya usafiri ya Algeria ilianguka mara tu baada ya kuondoka kutoka uwanja wa Ndege wa kijeshi wa Boufarik, kilomita 30 kusini mwa Algiers Jumatano Jana Jumatano. Watu 257 wamepoteza Maisha Katika Ajali ya ndege hii, kulingana na ripoti ya kwanza rasmi iliyotolewa na Wizara ya Ulinzi.

Ndege hii aina ya Iliouchine IL-76 ilianguka katika shamba moja karibu na uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik. Miongoni mwa waliopoteza maisha katika ajali hiyo ni askari na familia zao. Abiria 247 na wafanyakazi kumi wa ndege hiyo wote wameangamia katika ajali hiyo.

Ndege hiyo ilianguka katika "sehemu ya kilimo" muda mfupi baada ya kuondoka katika uwanja wa ndege wa kijeshi wa Boufarik huko Blida, kusini mwa Algiers.

Ndege hiyo ilikua ikielekea uwanja wa ndege wa kijeshi wa Tindouf, kwenye mpaka na Sahara Magharibi. Vyanzo vya Usalama, vilivyonukuliwa na gazeti la kila siku la Ennahar, vinabaini kwamba wajumbe 26 wa Polisario walikuwa katika ndege hiyo.

Mamlaka inajaribu kutafuta mabaki ya waliouawa. Picha kutoka eneo hilo zinaonyesha moshi ukifuka kutoka kwa vifusi vya mabaki ya ndege hiyo.

Naibu waziri wa Ulinzi, pia Mkuu wa majeshi ya Algeria, Jenerali Ahmed Gaid Salaha amezuru eneo la ajali.

Tume ya uchunguzi imeundwa ili kujua sababu ya ajali hiyo.


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Watu 257 wapoteza maisha katika ajali ya ndege ya kijeshi Algeria

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×