Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Serikali Kuchukua Hatua Kwa Vyombo Vya Habari Vitakavyotoa Tangazo Lenye Athari Kwa Jamii



Serikali imesema kuwa zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo Lenye Athari Kwa jamii hususani watoto.

Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza amesema hayo leo bungeni mjini Dodoma wakati akijibu swali la Mbunge wa Mororogo Kusini, Prosper Joseph Mbena kuhoji serikali kuwa kuongezeka kwa matangazo ya biashara kwenye vyombo vya habari upo baadhi ya matangazo hayo kuwakera na kuleta hisia tofauti kwa baadhi ya watu hasa watoto kutokana na maudhui mabaya ya baadhi ya matangazo hayo?


“Serikali tayari ina vyombo vya kusimamia maudhui ya vyombo vya habari nchini yakiwepo maudhui katika matangazo vyombo hivyo ni mamlaka ya Mawasiliano Tanzania(TCRA)ambayo iliundwa na Kamati ya Maudhui ya kifungu namba 26, Kamati hii inayosimamia maudhui na matangazo ya Kielekronic yaani redioni na Televisheni pamoja na mitandao ya kijamii,” amesema Shonza.

“Chombo cha pili ni bodi ya Filamu Tanzania ambayo inasimamia maudhui katika picha jengezi zinazoonyeshwa katika jumba la sinema, hadharani vilevile katika michezo ya kuigiza , Idara ya Habari Maelezo ni chombo cha tatu ambayo imewekwa chini ya kifungu cha sheria namba nne kifungu cha sheria ya habari namba 12 ya mwaka 2016 kinachosimamia maudhui katika machapisho mbalimbali yakiwemo magazeti, majarida pamoja na vipeperushi,”ameongeza.

“Zipo hatua mbalimbali zinazochukuliwa na serikali inapobainika bila kutia shaka kuwa kampuni au Taasisi imechapisha au kutoa tangazo lenye athari kwa jamii hatua hizo ni pamoja na kutoa onyo, kufungiwa, kufungiwa kutoa huduma kwa kipindi kitakachotajwa au kufungiwa kutojihusisha kabisa na utangazaji au uchapishaji wa habari pamoja na matangazo. Serikali inaendelea kuhimiza jamii nzima kuzingatia sheria na taratibu zilizopo katika kusambaza habari mbalimbali kwa jamii.”

Zanzibar24


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Serikali Kuchukua Hatua Kwa Vyombo Vya Habari Vitakavyotoa Tangazo Lenye Athari Kwa Jamii

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×