Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Zanzibar: Vifaa tiba vyaingizwa nchini , matumaini yaongezeka



Jumla ya Film za xree 1600 na madawa vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni nane vimetolewa kwa lengo la kusadia vituo vya afya , msaada uliyotolewa na Taasisi ya Abdalla Aid kupitia ZOPS ikiwa ni sehemu ya kupunguza tatizo la film katika Hospitali za kisiwa cha Pemba.

Akizungumza katika makabidhiano hayo huko katika hospitali ya chake chake muakilishi wa Taasisi ya Zanzibar Autreach Program kwa Pemba (ZOP) Abdalla Muhammed Mbaruk amesema kuwa baada ya kuona kuna upungufu wa vifaa hivyo katika hospitali za pemba ndipo walipoamua kuomba msaada kwa Abdalla Aid na kuweza kupatiwa filaam hizo .

Abdalla amesema kuwa fim hizo zimetolewa kwa ajili ya hospitali ya Chake Chake film600 ,hospitali ya Abdallah mzee mkoani film 500 hospitali ya wete 300 hospitali ya micheweni 100 pamoja na hospitali vitongoji 100

Kwa upande wake Naibu Mufti Zanzibar Mahmoud Mussa Wadi amesema kuwa aawashukuru viongozi wa Abdalla Aid kwa kuwapelekea maombi yao na wamewakubalia na kuwaletea msaada wa vifaa hivyo kwa wakati muafaka na wana waomba waendelee kuwafungulia misaada mengine pale watakapowaomba tena .

Naibu amesema kuwa msaada huo wa freem na dawa ambazo zitatumika na Taasisi ya ZOP kambi kwa hospitali za vijijini .

Waziri wa afya Zanzibar Hamad Rashid Muhammed amesema ni muhiu kwa taasisi kuunga mkono jitihada za serekali na kuamua ktoa mchango wao katika kuisaidia jamii .

Waziri hamad amewataka madaktari wawe na matumizi mazuri wa vifaa pamoja na madawa ili vipate kuwasaidia watu wenye mahitaji na sio kuviingiza madukani kwa ajili ya kuviuza.

Credit: Mzalendo


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Zanzibar: Vifaa tiba vyaingizwa nchini , matumaini yaongezeka

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×