Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

WANANCHI NDIO TUNAO SABABISHA AJALI, WALA SIO MAREVA WA BRT.

Habari za leo ndugu msomaji wa makala hii maalum iliyoandaliwa nasi na kuletwa kwako kupitia blog hii ya Tazama Line.


Leo naomba niweke wazi kabisa juu ya malalamiko ya wananchi hususani kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuhusu Mradi wa mabasi ya mwendokasi (BRT)

Tangu Mradi Huu umeanza kufanya kazi tayari zimekwisha tokea ajali nyingi sana nakatika ajali izo kuna magari mengi ya BRT yamealibika, kuna watu wamepoteza maisha na wengine ni waremavu hadi sasa, bila kusahau pikipiki, bajaji nk.


Ukisikiliza maoni ya mtu mmoja mmoja juu ya mradi huu wa BRT na ajali za barabarani, asilimia kubwa wanatupa lawama zote kwa mradi pamoja na  serikali nzima kwa ujumla.

Sisi binafsi tumegundua mapungufu ya mradi huu wa BRT, lakini sio kwa upande wa ajali za barabarani kama wananchi wanavyodai.

Ukweli nikwamba, watanzania wengi hawajui matumizi sahihi ya barabara, unakuta mtu/watu wanavuka barabara pasipokutumia eneo sahihi la Watembea Kwa Miguu (Zebra), wala bila kufuata taa za barabarani, na mambo mengine mengi.


Lakini kwa upande wa madreva wetu hapa nchini nao wapo kama wananchi ambao hawamiliki chombo chochote cha moto maana wao ndio wamekuwa msitari wa mbele kwa kuongoza kuchangia ajali nyingi barabarani hususani kwa njia ya BRT.

Kwenye majibu ya wengi utawasikia wakisema kwamba madreva wa mabasi ya mwendokasi wanatakiwa kusimama au kupunguza mwendo wa magari yao pindi wakiona wananchi wakivuka barabara ata kama hakuna zebra.


Je mbona kwenye usafiri wa Trein hatulalamiki kwamba trein inabidi isimame ili itusubirie sisi watembea kwa miguu pamoja na magari yetu tupite kwaza kisha ndipo iendelee na safari??

Hitimisho la makala hii kwa wananchi wa kawaida pamoja na madreva wote ni kwamba, sio kila kitu tuitupie lawama serikali vitu vingine nikujiongeza sisi wenyewe, tayari serikali ilisha kaa na kutoa suruhisho juu ya mradi huu ndio maana BRT inatumia barabara yake pekee kwaiyo mtu au kitu chochote kile kinapokiuka sheria za barabara ni haki yao kabisa madreva wa BRT kukugonga.




This post first appeared on Mutalemwa, please read the originial post: here

Share the post

WANANCHI NDIO TUNAO SABABISHA AJALI, WALA SIO MAREVA WA BRT.

×

Subscribe to Mutalemwa

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×