Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

KAMATI YA SIASA KATA YA KILIMANI YAKAGUA UJENZI WA SHULE



Na Barnabas Kisengi, Dodoma

Mapema leo Oktoba 11  2023 viongozi wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi  Kata ya kilimani  pamoja na wajumbe wa secretariat  ya kata ya kilimani    Wamefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa shule  ya msingi  unatekelezwa katika mtaa wa Chinyoyo kata ya Kilimani 

Pamoja na kuona kasi  ya ujenzi huo  unavyokwenda  viongozi hao  wamesisitiza ujenzi huo  uongeze kasi  kulingana na mkataba unavyoelekeza  licha ya kuwa na changamoto ndogo ndogo  ambazo  hazizuii mradi huo  kusimama.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Kata ya Kilimani Nathani Chibeye amesema ujenzi huo wa shule ya msingi hiyo utakuwa mkombozi kwa kata ya Kilimani kwa kuwa kata hiyo tangu ipate Uhuru haijawahi kuwa na shule ya msingi jambo ambalo hupelekea watoto wa mitaa minne ya Kilimani kusoma katika shule za kata nyingine na kusababisha kutembea umbali mrefu kuitafuta elimu.

"Hata hivi Sasa sisi kama viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani tunaishukuru SERIKALI YA AWAMU YA SITA INAYOONGOZWA NA RAIS SAMIA SULUHU  HASSAN kwa kuweza kutupatia fedha za ujenzi wa shule hii ambayo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kata ya kilimani"amesema Chibeye.

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Mapinduzi kata ya Kilimani Rotta Ndimbo ameitaka kamati ya ujenzi na mkandarasi kuhakikisha wanatanguliza uzalendo katika ujenzi wa shule hiyo ili thamani ya fedha zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi huo zinatumika kama zilivyo kusudiwa.

Ziara hiyo ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kata ya Kilimani ni mwendelezo wa kugagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na serikali katika kata ya Kilimani ili kuhakikisha utekelezaji wa ilani ya chama unafanikiwa.




This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

KAMATI YA SIASA KATA YA KILIMANI YAKAGUA UJENZI WA SHULE

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×