Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

UJUMBE MZITO WA MHE. STEPHEN MASELE AKISHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

 STEPHEN JULIUS MASELE: UJUMBE WANGU KWENU WAPIGANAJI LEO KATIKA SIKU YANGU YA KUZALIWA LEO TAREHE 01 OKTOBA 2023. 


Habari za leo ndugu zangu wapendwa? 

Ndugu zangu kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu sasa nimekuwa mtu mzima, busara na maarifa vimeongezeka,, na akili imekomaa zaidi na uzoefu na uvumilivu umeongezeka na  nimekomaa zaidi, nimekuwa kiumri na kiuongozi. Namtukuza Mwenyezi Mungu kwa zawadi hii muhimu ya afya na uhai. Tuzidi kumuomba yeye Mwenyezi Mungu kwani ndie muweza wa yote. 


Kiukweli ndugu zangu, Sina maneno mazuri zaidi ya kuelezea jinsi ninavyowapenda kwa dhati ya moyo wangu, nawapenda sana ndugu zangu, kwa namna tunavyoishi kwa kushirikiana kama familia moja, napenda umoja wetu uliojengwa kwa misingi ya upendo na kuta za ukweli na kuezekwa kwa paa ujasiri. 


Nafurahia maisha pamoja nanyi ndugu zangu. Leo katika siku yangu ya kuzaliwa Nataka nitamke kwamba ninyi ni sehemu ya familia yangu. Tumepitia magumu pamoja, ni wakati wetu sasa wa kujenga furaha ijayo kupitia umoja na mshikamano wetu, tuendelee kusaidiana kwenye shida na raha bila kubaguana.

 Natambua kwenye familia kubwa hapakosi tofauti za hapa na pale, tuendelee kuvumiliana kwani hakuna aliye mkamilifu kwani Mola wetu ametuumba tukiwa dhaifu. Tusisahau malengo yetu na malengo ya Chama chetu ni kushinda dola 2024/2025 kwa kushindo kwa nafasi za mitaa, udiwani, ubunge na Urais. 


Najua njia haitakuwa nyepesi, mawimbi na dhoruba zitakuwepo cha muhimu ni kushikamana pamoja na hakika tutashinda. Kwa pamoja tutashinda, kwa umoja wetu tutashinda, kwa nguvu zetu tutashinda. 


Chama chetu kinapaswa kuendelea kusimamia HAKI na UKWELI , kutengenezeana  ajali za kisiasa kunadhoofisha chama, tabia hii haikuwepo huko nyuma, najua sote mnajua tabia hii wapi ilikotoka, hatuwezi kukubali iendelee kwani itakivunja na kukisambaratisha chama. Hatuwezi kukubali uonevu, dhuruma na ubaguzi viendelee. 


Tutapigana mpaka tone la mwisho la damu kuhakikisha chama kinashinda chaguzi zijazo. Tunataka wana CCM shinyanga mjini warejee kwenye furaha kama zamani, natambua mioyo yenu inaumia sana lakini hamna la kufanya, nawaomba vumilieni. 


Hakika ukweli unaenda unajulikana, taifa litatambua na dunia itajua nini kimekuwa kikiendelea shinyanga mjini. Pongezi kwa chama kwa kufanya mabadiliko hivi karibuni, dhambi na uovu ulifunikwa na uongo unatoweka kwa uwezo wa Allah na Mungu wa mbinguni anasikiliza na kupokea maombi yenu, nawaambieni tutashinda vita, tutavuka pamoja. 


Namalizia kwa kusema msije hata siku moja mkakisaliti chama, kipiganieni chama kwa Nguvu Zenu Zote, kilindeni chama kwa nguvu zenu zote, bila chama wote hatuna heshima tulizonazo.


Msaidieni kusema mambo mazuri anayoyafanya Rais wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan, ana roho nzuri sana na upendo wa dhati kwa taifa lake, ni zawadi ya kipekee toka kwa Mungu, Muombeeni kwa Mungu ampe afya njema na maisha marefu na atuongoze vizuri zaidi. 


Nawaombea Mwenyezi Mungu awatunze ninyi na familia zenu. Nawapenda sana. 


Asanteni sana kwa salamu za kunitakia kheri ya siku yangu ya kuzaliwa. 


Wenu mtiifu, 

SM.





This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

UJUMBE MZITO WA MHE. STEPHEN MASELE AKISHEREHEKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×