Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

MERIDIANBET YAWAFIKIA WATU WASIOONA NA KUWAPA MSAADA!!


Maisha ya binadamu yamejaa mambo mengi sana, kuna mengi ya kidunia unaweza kupitia ukajiona hauna thamani tena kwa jamii, lakini uwepo wa Meridianbet umekuwa ni sehemu ya kurejesha matumaini kwa Watu Wenye Mahitaji ikiwemo watu wasioona.

Na kwa kuliona hili safari ya kutoka makao makuu ya Meridianbet wakali wa odds kubwa, michezo ya sloti na kasino ya mtandaoni walitembelea Jumuiya ya watu wasioona Tanzania, maeneo ya Kinondoni kutimiza mahitaji yao kuelekea “Maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fimbo Nyeupe” itakayofanyika Mkoani Njombe Tarehe 15 Oktoba.

Walijikuta na furaha kubwa iliyoambatana na machozi kwa kutokuamini kama ni kweli Meridianbet wameitikia wito wao na kuchangia pesa pamoja na mahitaji yao mengine.

Jamila Mohammed Mweka Hazina wa chama hicho alisema kuwa wana Zaidi ya wananchama 10,000/= mkoa mzima, na mahitaji yao kwa kiasi kikubwa ni fimbo.

“Tunahitaji fimbo kwaajili ya kutembelea, haya ni kama macho yetu sisi, hivyo mkituletea fimbo mtakuwa mmetusaidia kuona, Meridianbet tunawashukuru kwa hiki mlichotupatia sisi ni kikubwa kwetu na wadau wengine waige mfano huu”

Upande wa Meridianbet Amani Maeda alisema kwamba tangu kampuni hiyo imeanza kufanya kazi hapa nchini, imekuwa ikijihusisha na jamii kwa kutoa misaada mbalimbali haswa Kwa Watu Wenye mahitaji maalum.

“Tumetoa kidogo kwa jamii hususani ndugu zetu wasioona kuelekea siku ya kimataifa ya Fimbo nyeupe, lengo ni kuwawezesha kufika Njombe kuhudhuria tukio hilo lenye lengo la kuwaunganisha watu wasioona”-Amani Maeda

NB: Meridianbet wanakupa nafasi ya kuendelea kubashiri na kushinda kila unapojisajili, ili kubeti na kucheza kasino ya mtandaoni unapaswa kujisajili na kisha unapewa bonasi ya ukaribisho. Jisajili hapa.




This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

MERIDIANBET YAWAFIKIA WATU WASIOONA NA KUWAPA MSAADA!!

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×