Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

COUNSENUTH YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA KWA VIWANGO MIRADI WILAYANI CHEMBA




Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimtishwa Ndoo ya Maji Mwananchi mara baada ya kuzindua mradi wa Maji unaosimamiwa na Counsenuth wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo Cha Ushauri nasaha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.

Na. Gideon Gregory-CHEMBA

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Gerald Mongella amewahimiza wakazi wa kijiji cha Mrijo Juu Wilayani Chemba Mkoani Dodoma kuhakikisha wanatunza vyema kisima cha maji ambacho kimechimbwa kwa msaada wa kituo cha ushauri nasaha lishe na afya (CONSENUTH) kwa kushirikiana na nchi ya Ireland.

Mhe.Mongela ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kisima hicho ambapo amesema adui mkubwa ni yule atakaye kwenda kuchezea chanzo cha maji na kuongeza kuwa tayari visima 12 vimeisha chimbwa huku vitano vikiwa vimesalia kufikia jumla 17.

"Niwaelekeze jambo moja kati ya adui wenu mkubwa kuliko wote ni yule atakaye kuja kutaka kuchezea hiki chanzo cha maji, hiki chanzo cha maji mkitunze kwa nguvu zenu zote, CONSENUTH hawajachimba kisima kimoja bali vipo na vingine vitano kufikia 17,”amesema Mongela.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa CONSENUTH Shakila Mayumana amesema kuwa mradi wa lishe kijinsia katika mkoa wa Dodoma mpaka kufikia mwaka 2021 ulikuwa tayari umetekeleza afua zake katika vijiji vyote 114 vilivyopo Wilaya ya Chemba.

“Mradi wa lishe kijinsia mkoa wa Dodoma kufikia mwaka 2021 ulikuwa umefanikiwa kutekeleza afua zake katika vijiji vyote 114 vilivyokuwepo katika halmashauri ya wilaya ya Chemba,”amesema Mayumana.

Aidha ameongeza kuwa lishe za afya kijinsia pamoja na stadi za maisha na afya lishe vimetelelezwa katika shule za msingi 26 yaani kila shule moja kwa kila kata pamoja na afua ya kijinsia katika vijiji vyote.

Naye Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland Nancy Katalai amesema ubalozi wa nchi hiyo kwa muda mrefu umeelewa kuwa sababu za lishe duni na athari zake zinahusiana kwa karibu na sifa za kitamaduni ikiwemo kaya na jamii ambapo wanawake wanakosa mamlaka ya kufanya maamuzi ndani ya nyumba.

Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akizungumza wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma


Mkurugenzi Mtendaji wa Counsenuth Bi.Shakila Mayumana,akitoa taarifa ya Mradi wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma


Mwakilishi wa Ubalozi wa Ireland Bi.Nancy Katalai,akizungumza wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma


Mtendaji wa Kata ya Mrijo Juu Bi.Jesca Njinga,akisoma risala wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma



Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella (hayupo pichani) wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma


Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akizindua mradi wa Maji unaosimamiwa na Counsenuth wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma


Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimtishwa Ndoo ya Maji Mwananchi mara baada ya kuzindua mradi wa Maji unaosimamiwa na Counsenuth wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akimkabidhi hati ya Kiwanja Mkurugenzi Mtendaji wa Counsenuth Bi.Shakila Mayumana, wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma



Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akiwakabidhi zawadi washindi wa michezo mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.


Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe.Gerald Mongella,akiwa katika picha mbalimbali wakati wa maadhimisho ya mafanikio ya mradi wa lishe kijinsia Chemba unaosimamiwa na Kituo cha Ushauri na Saha Lishe na Afya (Counsenuth) uliofanyika wilayani Chemba Mkoani Dodoma.


This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

COUNSENUTH YAPONGEZWA KWA KUTEKELEZA KWA VIWANGO MIRADI WILAYANI CHEMBA

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×