Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Picha : SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA LISHE NA WIKI YA UNYONYESHAJI, RC MNDEME ASISITIZA ZIWA LA MAMA NI UHAI WA MTOTO



Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme amewataka akina mama kuhakikisha wanawanyonyesha watoto wao mara kwa mara kadri wanavyotaka huku akisisitiza kuwa kunyonyesha maziwa ya mama pekee miezi sita ya mwanzo ya maisha ya mtoto ndiyo njia bora na salama ya kumpatia virutubisho vyote muhimu kwa ukuaji na maendeleo ya mtoto.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito huo leo Jumamosi Agosti 5,2023 wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga ambapo pia ameongoza zoezi kupima uzito na urefu sambamba na kuwapatia watoto chakula chenye lishe.


“Kama tunavyofahamu unyonyeshaji wa maziwa ya mama huchangia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha afya, kulinda uhai na maisha ya mtoto. Wataalamu wetu wanashauri Mtoto anyonyeshwe ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ili kusaidia maziwa yatoke mapema lakini pia Mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama pekee bila ya chakula na kinywaji kingine (hata maji) katika miezi sita ya mwanzo”,amesema Mhe. Mndeme.


Ameeleza kuwa maziwa ya mama yana sifa ya kipekee ya kuwa na kinga ya mwili ambayo humkinga mtoto dhidi ya magonjwa, hivyo kuchangia kupunguza vifo vya watoto chini ya umri wa miaka mitano na kujenga mahusiano mazuri kati ya mama na mtoto wake.


“Mtoto anyonye mara kwa mara kadri anavyohitaji ili maziwa yatoke kwa wingi na ya kutosha. Mnyonyeshe mtoto wako titi moja kwanza mpaka alale au aachie mwenyewe ndipo umpe titi lingine ili ashibe na asiwe analialia. Usimnyang’anye mtoto ziwa mdomoni, ziwa la mama ni hoteli ya mtoto”,amesema Mhe. Mndeme.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa amembeba mtoto aliyenyonyeshwa miezi sita bila kupewa chakula kingine.
“Usimwachishe mtoto kunyonya kwa sababu ya ujauzito; endelea kumnyonyesha Mtoto mpaka mimba ifikishe miezi saba (7). Mtoto anapofikisha miezi sita (6), aanzishiwe vyakula vya nyongeza lakini aendelee kunyonyeshwa maziwa ya mama hadi atimize miaka miwili (2) au zaidi”,ameongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Amefafanua kuwa ili kufanikisha unyonyeshaji kama mkakati mojawapo wa kuboresha lishe ya watoto, jamii yetu inashauriwa kuwa baba anao wajibu wa kumpunguzia mama kazi wakati wa ujauzito na wa kunyonyesha ili kuboresha Afya ya mama na mtoto na familia imsaidie mama aweze kunyonyesha mtoto maziwa yake pekee bila hata maji kwa miezi sita ya mwanzo.


“Tunaelewa wazi kuwa pamoja na upimaji maendeleo ambayo Mkoa wetu umekuwa ukiyapata katika maeneo mbalimbali, bado utapiamlo umeendelea kuathiri jamii hususani katika nyanja za afya, elimu na uchumi; hivyo kusababisha kasi ya kupungua kwa umaskini kutoridhisha”,ameongeza.

Amesema lishe duni si tu inaathiri maendeleo ya mtoto lakini pia inaathiri ukuaji wake kimwili na kiakili hatimaye kuathiri mchango wake katika maendeleo ya Taifa kwa kipindi chote cha uhai wake.

“Utafiti wa kitaifa uliofanyika hivi karibuni, mwaka 2022, unaonesha kuwa kiwango cha Udumavu kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika Mkoa wetu kimepungua kutoka asilimia 32.1 mwaka 2018 hadi kufikia asilimia 27.5 mwaka 2022. Sababu kubwa ya utapiamlo huu kwa watoto ni ulishaji usio sahihi ambao huchangiwa na majukumu mengi yanayomkabili mama na hivyo kukosa muda wa kutosha wa kumtunza mtoto”,ameeleza.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Amesema Serikali inatambua kuwa bado zipo changamoto nyingi katika kukabiliana na utapiamlo hapa nchini ambapo changamoto kubwa kuliko zote ni ile ya uelewa mdogo wa masuala ya lishe katika jamii ikiwemo unyonyeshaji, kuanzia ngazi ya familia hadi kwa watendaji na viongozi wa Serikali.

Amesema uelewa mdogo kuhusu masuala ya lishe pia umesababisha masuala ya lishe kutopewa kipaumbele katika jamii ambako ndiko waliko watoto na wanawake wengi wanaohitaji zaidi huduma bora za lishe.


“Ili kuhakikisha kuwa lishe inaendelea kuimarika katika Mkoa wetu, natoa wito kwa watendaji wa kata, vijiji na mitaa ndani ya Mkoa wa Shinyanga kuhakikisha mnasimamia na kuadhimisha Siku za Afya na Lishe za Vijiji/Mitaa kila robo mwaka (miezi 3) kwa kushirikiana na wataalamu wa afya na lishe ngazi zote ili kutoa elimu kwa wananchi wote”,amesema Mkuu wa Mkoa.


“Aidha, natoa wito kwa wananchi wote kuzingatia ushauri wa kitaalamu unaotolewa ili kuboresha lishe na afya ya mama na mtoto. Kwa kufanya hivyo kizazi chetu kitakuwa salama, na hivyo kuongeza uzalishaji”,amesema.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto.

Katika hatua nyingine amesema nchi ya Tanzania imechukua hatua mbalimbali kuendeleza unyonyeshaji ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini ya mwaka 2004 inayotambua kuwa unyonyeshaji ni haki ya mtoto na hivyo hutoa mafao mbalimbali ya uzazi ili kuwawezesha wazazi kumlea mtoto hususani kumnyonyesha ipasavyo.


Ameeleza kuwa Mama mwajiriwa anayenyonyesha hupewa ruhusa ya masaa mawili kila siku ili akamnyonyeshe mtoto wake. Pia, sheria hiyo hutoa fao la likizo ya uzazi kwa mama na baba wa mtoto. Mama anapata likizo ya siku 84 kama amejifungua mtoto mmoja na siku 100 kwa watoto zaidi ya mmoja. Sheria hii pia humpa baba likizo ya siku 5 ndani ya wiki moja aliyojifungua mama.


“Aidha sheria hiyo inakataza mama aliye ajiriwa na ambaye ananyonyesha au mjamzito kufanya kazi ngumu au za hatari kwa afya yake au ya mtoto wake. Kwa sababu hii, tunatoa wito kwa Taasisi zisizo za kiserikali, Taasisi za kijamii, kidini, jamii yenyewe na familia kwa ujumla kuwasaidia wanawake ambao hawapo kwenye ajira rasmi ili waweze kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo”,ameongeza Mhe. Mndeme.


Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungile amesema Maadhimiho ya Siku ya Lishe Mkoa Shinyanga yanalenga kuhamasisha na kutoa elimu ya lishe kwa jamii ikiwa ni mkakati wa kupunguza udumavu kwa watoto chini ya miaka 5.

“Maadhimisho haya yana lengo la kutoa elimu ya ulishaji wa watoto wadogo na wachanga ikiwemo kusisitiza unyonyeshaji wa maziwa ya mama pekee kwa miezi sita (6) ya mwanzo ya maisha ya mtoto lakini pia kuhamasisha jamaii kuzingatia Lishe bora ili kuwa na afya imara”,amesema Dkt. Ndungile.


“Leo tunaadhimisha siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga ambayo inalenga kuongeza uelewa kwa wananchi juu ya Lishe tukiongozwa na kauli mbiu "Saidia unyonyeshaji, wezesha wazazi kulea watoto na kufanya kazi zao kila siku". Lakini pia tunaadhimisha Wiki ya Unyonyeshaji inayoadhimishwa Duniani kote kila mwaka kuanzia tarehe 01 hadi 07 Agosti ambayo imekuwa ikifanyika tangu mwaka 1992 ikilenga kusisitiza umuhimu wa kulinda, kuendeleza na kusaidia unyonyeshaji na ulishaji bora wa watoto”,amesema Dkt. Ndungile.


Amesema Wiki ya unyonyeshaji Duniani hutoa fursa maalum kwa watu wote kuungana pamoja katika kukumbushana umuhimu wa kuendeleza na kuimarisha unyonyeshaji maziwa ya mama kama njia bora zaidi ya kujenga afya ya mama na mtoto kimwili na kiakili

 ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga - Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 akizungumza wakati wa Maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yamefanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga. Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Yudas Ndungule akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji yaliyofanyika leo Jumamosi Agosti 5,2023 katika Soko la Ndala Manispaa ya Shinyanga
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamis akielezea kuhusu masuala ya lishe na unyonyeshaji wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Afisa Lishe Manispaa ya Shinyanga Amani Mwakipesile akielezea kuhusu makundi ya vyakula wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Burudani ya ngoma za asili za kucheza na nyoka ikiendelea kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Diwani wa kata ya Ndala Zamda Shaban akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akichenza muziki (Kwaito) na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy COM) wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (aliyevaa nguo nyeusi) akicheza muziki (Kwaito) na Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy COM) wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji. Katikati aliyevaa suruali ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akimpa zawadi mtoto aliyenyonyeshwa miezi sita bila kupewa chakula kingine na mama yake (aliyeshikilia kipaza sauti) wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akimpa zawadi mtoto aliyenyonyeshwa miezi sita bila kupewa chakula kingine na mama yake wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Loveness Jameson akionesha namna ya kumuweka mtoto wakati wa kunyonyesha . Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme
Lydia Bryson akielezea faida za kunyonyesha mtoto miezi sita bila kumpa chakula kingine wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipima Shinikizo la damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipima Shinikizo la damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipima uzito wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akipima urefu wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipima Shinikizo la damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipima Shinikizo la damu wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Watalaamu wa afya wakimuelezea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kuhusu vipimo vya urefu na uzito
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akipima uzito wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akigawa uji wenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza baada ya kugawa chakula chenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza baada ya kugawa chakula chenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Diwani wa kata ya Ndala, Mhe. Zamda Shaban akitoa neno la shukrani baada ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kugawa chakula chenye lishe kwa watoto wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wanafunzi wa Chuo cha Ualimu Shinyanga (Shy com) wakiwa kwenye kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi na wanafunzi wa chuo cha ualimu Shinyanga (Shy Com) wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji
Wananchi wakiwa kwenye maadhimisho ya siku ya Lishe Mkoa wa Shinyanga na Wiki ya Unyonyeshaji.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blog




This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

Picha : SHINYANGA WAADHIMISHA SIKU YA LISHE NA WIKI YA UNYONYESHAJI, RC MNDEME ASISITIZA ZIWA LA MAMA NI UHAI WA MTOTO

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×