Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

YANGA YAPOTEZA TENA NIGERIA


WAWAKILISHI wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa, Yanga leo jitihada zao za kupindua meza kimataifa zimekwama nchini Nigeria kwa kuwa wamefungwa tena.

Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi wa zaidi ya bao 1-0 kwa kuwa katika mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa ilikubali kupoteza kwa kufungwa bao 1-0.

Leo pia ugenini nchini Nigeria Yanga imepoteza kwa kufungwa bao 1-0 hivyo wametolewa kwa jumla ya mabao 2-0.

Safari yao na malengo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yameyeyuka mazima hivyo wanarudi Dar es Salaam.

Haji Manara, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wamefanyiwa vitendo vya kihuni na wapinzani wao hasa kwenye suala la vipimo vya Corona.

"Tumefanyiwa mambo ya kihuni na tumepewa matokeo ya Corona dakika 45 kabla ya mchezo huu ni uhuni,".


This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

YANGA YAPOTEZA TENA NIGERIA

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×