Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YATOA MAAMUZI HATMA YA DHAMANA YA MBUNGE SULEIMAN NCHAMBI

Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga leo Ijumaa Mei 15,2020 imetoa maamuzi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kishapu mkoa wa Shinyanga Suleiman Nchambi (CCM) anayeshtakiwa kwa makosa 12 ya Uhujumu Uchumi ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti.

Akitoa maamuzi ya maombi ya dhamana hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga Phocus Mkeha, ambaye alikuwa akisikiliza maombi ya dhamana hiyo amesema Mbunge huyo ana haki ya kupewa dhamana kwa masharti ya kusaini bondi ya Shilingi Milioni 50, na mdhamini wake bondi ya Milioni 10, pamoja na kushikiliwa Hati yake ya kusafiria 'Passport'.

Aidha amesema maamuzi ya utoaji wa dhamana hiyo ameyarudisha katika mahakama ya wilaya ya Shinyanga mahali kesi yake ya msingi ilipoanzia ambapo wao ndiyo watasimamia masharti ya utoaji wa dhamana hiyo.

Soma Pia : OMBI LA DHAMANA KESI YA MBUNGE WA KISHAPU MHE. NCHAMBI LASIKILIZWA MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA

Soma pia : MBUNGE WA Kishapu Suleiman Nchambi KUENDELEA KUSOTA RUMANDE..KESI YAKE YA UHUJUMU UCHUMI YAPIGWA KALENDA HADI MEI 25

MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UHUJUMU UCHUMI

MBUNGE WA KISHAPU SULEIMAN NCHAMBI AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUKUTWA NA SILAHA 10, RISASI 536 NA NYAMA 'UWINDAJI HARAMU'



This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

MAHAKAMA KUU KANDA YA SHINYANGA YATOA MAAMUZI HATMA YA DHAMANA YA MBUNGE SULEIMAN NCHAMBI

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×