Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

TANESCO yapata hasara ya bilioni 189!

Shirika la Umeme nchini, TANESCO, limekuwa likipata hasara ya kati ya shilingi bilioni 109 na bilioni 189 kwa kila mwaka Katika Kipindi Cha miaka mitatu iliyopita kutokana na kuuza umeme kwa bei nafuu.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nishati na Madini, Mhesmiwa William Ngeleja wakati akijibu swali la Mbunge wa Mlalo, CCM, Brigedia Jenerali (mstaafu) Hassan Ngwilizi.

Mheshimiwa Ngwilizi alitaka kujua kwanini bei za umeme zinazidi kupanda badala ya wananchi kufaidika na raslimali zilizopo nchini.

Akijibu swali hilo , Mhesimiwa Ngeleja akasema kuwa hasara hiyo ilipatikana katika kipindi cha kati ya mwaka 2004 na mwaka jana.

Akasema katika miaka ya nyuma, Serikali ilikuwa ikiipatia Tanesco ruzuku kwa ajili ya kufidia tofauti kati ya bei ya kuuzia umeme na gharama halisi za umeme nchini.

Hata hivyo, akasema kuanzia mwaka wa fedha wa 2007 na 2008, Serikali imesitisha utoaji wa ruzuku kwa shirika hilo na kuridhia kuwa bei za umeme ziwe zinarudisha gharama halisi za umeme.

Akafafanua kuwa inapaswa sasa shirika hilo lijiendeshe kibiashara na kuwa kutokana na hatua hiyo chanzo pekee cha mapato ya shirika hilo ni uuzaji wa umeme.

SOURCE: Alasiri, 22/4/2008



This post first appeared on Godfreyenergy, please read the originial post: here

Share the post

TANESCO yapata hasara ya bilioni 189!

×

Subscribe to Godfreyenergy

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×