Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Zanzibar yatambuliwa rasmi CAF

Shirikisho la soka Afrika (Caf) limeridhia kuipa uanachama wa kudumu Zanzibar kuanzia leo.
Ombi hilo limeridhiwa na mkutano mkuu wa Caf unaondelea huko Addis Ababa, Ethiopia.
"Ombi la Zanzibar limepita bila kuwekewa pingamizi. Zanzibar sasa ni mwanachama wa 55 wa Caf, " uliandika ukurasa wa Twitter wa shirikisho hilo.
Kwa kupata nafasi hiyo, no rasmi sasa timu ya taifa na Zanzibar itapata fursa ya kushiriki mashindano yote yanayoandaliwa na Caf.
Zanzibar sasa itaweza kushiriki mashindano yanayoandaliwa na CAF kama vile Mataifa ya Afrika (AFCON), fainali za Afrika Wanawake (AWCON), fainali za vijana (AFCON U17 na AFCON 20).
Pia, itakuwa na uhalali wa kuhudhuria mikutano mbalimbali sanjari na kupokea na kusimamia kozi mbalimbali na kupata fursa ya ya kupiga kura katika masuala muhimu ya CAF.
Hivi sasa Zanzibar inapata fursa ya klabu zake zinazoshika nafasi ya juu katika Ligi Kuu ya Zanzibar kushiriki Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Zanzibar yatambuliwa rasmi CAF

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×