Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Nape aipa tano kurugenzi mawasiliano Ikulu, habari maelezo

Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amezipongeza Kurugenzi za Mawasiliano Ikulu na Idara ya Habari Maelezo kwa ubunifu wanaouonesha katika kuelezezea mafanikio ya Serikali kwa Kutumia Teknolojia Mbalimbali za habari na mawasiliano.
Nape ametoa kauli hiyo siku moja baada ya kumwagiza mkurugenzi wa habari maelezo, kufuatilia utendaji kazi wa maofisa habari na mawasiliano wote ili kuona kama utendaji wao unaleta tija kwa jamii.
Akizungumza leo (Jumatano) Waziri Nape amesema licha ya changamoto ya vifaa vinavyowakabili maafisa mawasiliano wa Serikali, kurugenzi za mawaziliano Ikulu na idara ya habari maelezo wamekuwa wanafanya kazi nzuri za kuisaidia Sarikali.
“Nawapongeza wakurugenzi vijana, Dk Hassan Abbasi (Maelezo) na Grayson Msigwa wa Ikulu. Hawa ni mfano wa ubunifu wa namna Serikali inavyoweza kutumia teknolojia mbalimbali za mawasiliano katika kuhakikisha mazuri yanayofanywa na Serikali yanatangazwa, yanaenezwa na kutetewa,”amesema Nape.This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Nape aipa tano kurugenzi mawasiliano Ikulu, habari maelezo

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×