Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mbunge akabidhi gari la wagonjwa

Tags: katika gari afya

MBUNGE wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Simiyu, Mashimba Ndaki (CCM) amekabidhi Gari la kisasa la kubeba wagonjwa kwa Kituo cha Afya cha Malampaka kilichopo Tarafa ya Sengerema wilayani humo.
Gari hilo lenye thamani ya Sh milioni 200, ni miongoni mwa magari 50 yaliyotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Shirika la Afya Duniani (WHO) kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Gari hilo la wagonjwa limekabidhiwa jana katika hafla iliyofanyika katika kituo hicho ambalo litakuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na hapo awali walikuwa wanapata usumbufu pindi wanapoumwa kutokana na upatikanaji wa gari kuwa mgumu.
Akizungumza na wananchi wa tarafa hiyo baada ya kukabidhi msaada wa gari hilo la wagonjwa, Ndaki alisema magari kama hayo yametolewa katika maeneo mbalimbali ya nchi hasa mikoa ya Kanda ya Ziwa na gari moja pekee ndilo limetolewa kwa wananchi wa jimbo hilo.
Aliipongeza Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli ambayo iliahidi kutatua changamoto ya kero ya vifo vya wajawazito ambavyo vilikuwa vikitokea kutokana na eneo hilo kukosa gari la wagonjwa.
“Kutokana na huduma hafifu ya rufaa kwa wajawazito kwa kukosa magari ya wagonjwa, ukosefu wa damu salama na ushiriki mdogo wa jamii katika mambo yanayohusu afya ya mama, ikiwemo kutotambua dalili hatari wakati wa ujauzito za kuokoa maisha ambayo yanachangia wingi wa vifo vitokanavyo na uzazi hivyo serikali imeona umuhimu wa kutupatia gari hili,” alisema mbunge huyo.
Alisema shida waliyokuwa wakiipata kwa muda mrefu wananchi wa tarafa hiyo hasa ya usafiri pindi wanapokuwa wagonjwa na wengine kusafirishwa kwa kutumia magari ya kukodi kwa Sh 120,000 huku wengine wakilazimika kutumia matela yanayokokotwa na ng’ombe, sasa itakuwa historia.
Aidha, aliongeza kuwa nia yake kubwa mbali na kupata msaada huo wa gari la wagonjwa pia atahakikisha anaboresha sekta ya afya katika jimbo katika zahanati na vituo vyote vya afya ili kuwapa fursa wananchi wapate huduma ambayo inastahili pamoja na matibabu.
Pia alisema anapambana vilivyo kuhakikisha kunakuwepo na vifaa vya tiba katika maeneo husika pamoja na kuongeza idadi ya wauguzi, kwani anatambua bado kuna changamoto nyingi katika sekta ya afya hivyo atajitahidi kadiri ya uwezo wake ili kuongeza kasi ya kuboresha huduma hiyo ya afya.
Mkazi wa Kijiji cha Malampaka, Jamila Hamis aliishukuru serikali kutokana na kuwepo kwa kilio cha siku nyingi cha wananchi kutozwa gharama kubwa ya usafiri.
“Leo serikali imesikia kilio chetu cha muda mrefu kwani tulikuwa tunatozwa kiasi kikubwa cha fedha kati ya shilingi laki moja hadi shilingi laki moja na ishirini kwa kutumia magari ya watu binafsi pindi unapokuwa na mgonjwa unapotakiwa kumleta katika kituo chetu cha afya au hata akipata rufaa ya kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambayo iko umbali wa kilometa thelathini na nane. Sasa kuanzia mwezi huu hiyo kilio hicho hakitakuwepo tena,” alieleza.
Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dk Vedastus Luguga alisema kipindi cha nyuma wagonjwa walikuwa wanapata shida kubwa ya usafiri na wakati mwingine walishindwa kwenda kupatiwa matibabu kwa muda wa muafaka na kusisitiza kuwa hakuna mwananchi yeyote atakayetozwa gharama katika kutumia gari hilo.



This post first appeared on HABARI ZA SIASA NA MUZIKI, please read the originial post: here

Share the post

Mbunge akabidhi gari la wagonjwa

×

Subscribe to Habari Za Siasa Na Muziki

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×