Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

CHAKULA UNACHOTUMIA NI MUHIMU KWA UWEZO WAKO WA KUONA

chakula muhimu kwa uwezo wa kuona

Macho ni kiungo pekee mwilini kinachokuwezesha kuitambua dunia na vilivyomo.  Kuongezeka kwa mahitaji ya binadamu kunakosababishwa na kukua kwa uchumi kunaongeza muda ambao Macho yanakuwa kazini.

Taka zinazotokana na uchafuzi wa mazingira, muda mrefu wa kufanya kazi kwenye kompyuta na matumizi yaliyokithiri ya simu za mkononi huchukua muda mwingi wa macho kuendelea kutumikishwa.  Licha ya haya yote, bado watu wengi hawali vyakula muhimu kwa afya ya macho yao.  Ama hawafahamu au hawajui kuwa chakula hasa virutubisho vilivyomo ni muhimu Kwa Ajili ya kulinda uwezo wa macho kuona hata kwa wenye umri mkubwa.

Kitu muhimu ambacho wataalam wa masuala ya macho wanapendekeza ni kutambua ukweli kwamba uwezo wetu wa kuona hutegemea aina ya vyakula tunavyotumia kila siku.

Kanuni

Upo ushauri rahisi ambao wataalam wa macho wanashauri kila mmoja kuuzingatia.  Uchunguzi wa macho wa mara kwa mara hata kama hakuna dalili hatarishi zilizojitokeza.

Wataalam wanasema vipimo hivi vinaweza kusaidia kugundua tatizo ambalo dalili zake hazijaanza kujitokeza na kupendekeza matibabu yatakayozuia madhara yake.  Maradhi haya yanaweza kuwa presha ya macho au glaucoma ama matatizo ya lensi ya jicho au cataracts.

Wanashauri kufanya vipimo vya macho kila baada ya miaka miwili ingawa daktari wako anaweza kupendekeza vinginevyo.

Macular degeneration; maradhi ya kupoteza uwezo wa kuona kadiri umri unavyozidi kusogea ni tatizo linalowakabili watu wengi ulimwenguni lakini yakibainika mapema mgonjwa anaweza kuishi vyema.

Kwa wanaopenda masuala ya urembo hasa wa macho, wanashauriwa kuepuka vipodozi vilivyokwisha muda wake kwani vinaweza kusababisha maambukizi na kuleta madhara makubwa kwa mhusika.

Vyakula
Ulaji wenye mpangilio una manufaa kwa ufanisi wa macho yako, kinachotakiwa ni mchanganyiko makini wa vyakula muhimu kwenye mlo wako.

Mlo wenye matunda mengi na mboga za majani vinahitajika Zaidi Kwa Ajili ya afya ya macho yako.  Umuhimu wake huonekana zaidi virutubisho hivi vinapoimarisha kinga za mwili na kupambana na seli zilizokufa (free radicals).

Mboga za majani hasa zenye kijani kibichi ndizo zinazoshauriwa zaidi kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa uendelevu wa macho kuona.  Spinachi, matembele au kisamvu ni baadhi ya mboga hizo.

Wataalam wanashauri kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi au sukari nyingi ingawa mafuta mazuri yanashauriwa.  Yanayopendekezwa ni yale ya samaki…hakikisha unakula mafuta mengi ya samaki kila wiki, ukiweza.

Licha ya mafuta ya samaki, ya karanga na mazao mengine ya jamii ya njugu pia yanapendekezwa kwa ajili hiyo.  Matunda hasa maparachichi ni chanzo kingine cha virutubisho muhimu vya uimara wa macho.

Kubadili mfumo wa maisha hasa kwa kuepuka au kupunguza uvutaji wa sigara na bidhaa nyingine za tumbaku kunashauriwa ili kukinga hatari zinazoweza kujitokeza.  Inashauriwa kuepuka mionzi ya UV (Ultraviolet rays).

Madini na Virutubisho

Inashauriwa kuhakikisha kwenye kila mlo kunakuwa na antioksidanti (antioxidants) hasa lutein na zeaxathin kutokana na umuhimu wake wa kulilinda jicho kupoteza uwezo kwa sababu ya umri mkubwa (macula) au hitilafu za lensi ya jicho (cataracts).

Lipo tatizo kubwa la kuwa na macho makavu hasa miongoni mwa wanawake ambao kipindi chao cha hedhi kimekoma.  Mafuta ya samaki wa baharini ni suluhisho la tatizo hili.  Yana wingi wa virutubisho vya omega 7 ambavyo husaidia kurudisha vilainishi vya macho, yakiwamo machozi.

Kupata virutubisho hivi, unashauriwa kutumia zaidi mafuta ya samaki endapo yatakosekana basi siyo mbaya ukitumia aside za fati (fatty acids) zinazouzwa kwenye maduka ya dawa.


This post first appeared on Afya Na Kiasi, please read the originial post: here

Share the post

CHAKULA UNACHOTUMIA NI MUHIMU KWA UWEZO WAKO WA KUONA

×

Subscribe to Afya Na Kiasi

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×