Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

UNAHITAJI UMAKINI ZAIDI UNAPOKUWA MJAMZITO KUANZIA MIAKA 35


ujauzito zaidi ya miaka 35Ingawa hakuna Umri maalamu ambao mwanamke anaweza kushika ujauzito baada ya kukidhi vigezo vya kibaiolojia, tunafahamu kwamba kuanzia miaka 35 uwezo huo hupungua na changamoto za uzazi huongezeka.
Japokuwa hilo sio lazima litokee kwa watu wote kwani wapo wanawake ambao hupata ujauzito wakiwa na miaka 40 na 50 bila tatizo lolote, ushauri wa daktari au mkunga ni muhimu kwa watu wa Umri Huo.
Kutokana na mfumo wa elimu na matakwa ya kitaaluma, wanawake wengi huchelewa kuzaa miaka hii licha ya ukweli kwamba uzazi kwao una mipaka inayozingatia umri na uwezo wa mwili kutimiza matakwa hayo.
Japokuwa haimaanishi tatizo la kiafya kwa mwanamke anayeamua kuzaa baada ya umri huo, kuna masuala kadhaa ya kuzingatia ili kupunguza changamoto zinazoweza kujitokeza.
Kila mwanamke anayo idadi maalamu ya mayai ambayo huzaliwa nayo.  Mayai haya hupungua kadri umri unavyoenda.  Kuanzia miaka 30 na 40, idadi na ubora wa mayai haya hupungua.  Kupungua kwa ubora wa mayai yako kunaongeza ugumu wa kupata ujauzito kwa wakati ingawa si wakati wote.
Ukiacha haya, zipo changamoto ambazo mwanamke anayetaka kushika ujauzito baada ya miaka 35 anapaswa kuzizingatia na kufuata ushauri wa daktari au mkunga atakayemuwezesha kukabiliana nazo.
Pacha
Uwezekano wa kuzaa pacha huongezeka kadri umri unavyosogea.  Uzoefu unaonesha, mjamzito wa zaidi ya miaka 35 yupo kwenye uwezekano wa kuzaa pacha watatu.
Kwa wale wanaotumia dawa za kutafuta mimba uwezekano huo huongezeka Zaidi.  Kuwa na ujauzito wa aina hii kwa umri huo huambatana na changamoto kadhaa zinazophitaji uangalizi wa daktari ili kuepuka kujifunza kabla ya wakati, kifafa cha mimba na kisukari cha mimba.
Magonjwa
Uwezekano wa kuugua kisukari cha mimba huongezeka kwa wajawazito wa umri huo.  Ili kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza, mjamzito atapaswa kuzingatia masharti ya chakula ili kutozidisha kiasi cha sukari kwenye damu yake.
Hii inaweza kuhitaji matibabu endapo hali itakuwa mbaya.  Hatua za maksudi zisipochukuliwa kutibu kisukari hiki kitaathiri ukuaji wa mtoto au watoto watakaozaliwa na maisha yake hapo baadae.
Shinikizo la damu kwa wajawazito wa umri huu ni kawaida pia.  Uangalizi wa daktari na matibabu ni muhimu kwao vilevile.
Njiti
Upo uwezekano wa kujifungua kabla ya muda hivyo mtoto au watoto wakawa njiti na wenye uzito mdogo.  Kwa kawaida, mtoto aliyezaliwa kabla ya majuma 37 ya ujauzito, kitabibu, huwa njiti.  Watoto hawa huwa na changamoto kadhaa ambazo zinahitaji umakini kuwatunza mpaka wakue.
Upasuaji
Upasuaji ni suala jingine ambalo mjamzito wa umri mkubwa anashauriwa kama njia ya kujifungua.  Kadri umri unavyoenda ndivyo matatizo ya kujifungua kwa njia ya kawaida yanavyoongezeka.
Matatizo ya mara kwa mara ni kujiviringa kwa kitovu cha mtoto jambo linalohatarisha maisha yake hivyo huhitaji upasuaji.
Matatizo ya Kuzaliwa Nayo
Ingawa ni nadra, wanawake katika umri huo wapo kwenye hatari ya kujifungua watoto wenye matatizo ya chembembuzi au chromosomal abnormalities ambayo husababisha ugonjwa uitwao down syndrome (DS).
Inaelezwa, DS hutokea kwa mtoto mmoja kati ya vizazi 700, mara nyingi kwa wanawake wenye umri mkubwa ingawa hata walio chini ya miaka huweza kujifungua.
Watoto hawa pia wanaelezwa, kuwa na uwezekano wa kuzaliwa na matatizo ya moyo.  Tatizo jingine ambalo linaweza kujitokeza ni kuharibika kwa mimba.  Wanawake wa umri huo, wana hatari ya mimba zao kuharibika.
Licha ya changamoto hizi zilizoelezwa bado zipo namna za kuweza kuishi na ujauzito na kujifungua salama.  Kujali afya kwenye kipindi chote cha ujauzito kwa ajili ya afya ya mama na mtoto ni muhimu bila kujali umri.
Mimba Salama
Kabla ya kupata ujauzito, wanawake wenye umri huu wanashauriwa kupata maelekezo ya daktari na kufahamu mambo muhimu wanayotakiwa kuyazingatia.  Ushauri kuhusu namna ya kurahisisha kushika mimba, lishe kwa kipindi hicho na historia na maradhi ni muhimu kwa wanawake hawa.
Kuhudhuria kliniki ni muhimu kwa wajawazito wote ila zaidi kwa wenye umri huo.  Wajawazito hawa wanapaswa kuzingatia hili kwa ajili ya afya zao na watoto wanaotarajia kujifungua.
Lishe bora ni suala jingine muhimu.  Wakati wa ujauzito, wanawake wanahitaji vitamin D, folic acid, calcium na virutubisho vingine.  Wanashauriwa kunywa maji mengi na kula mlo kamili wenye matunda na mboga za majani kwa wingi.
Ingawa huwa kunakuwa na uchovu, kufanya mazoezi ya viungo ni muhimu.  Haya husaidia kufungua njia ya uzazi na kupunguza uwezekano wa kufanyiwa upasuaji.
Mazoezi pia husaidia kuimarisha afya ya mwili mzima.  Kila program mpya ya mazoezi unayoifanya ni lazima iruhusiwe na daktari wako anayekuchunguza katika kipindi hiki kabla hujaianza.
Achana na vitu vinavyohatarisha afya.  Unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara pamoja na dawa za kusisimua mwili ni miongoni mwa mengi usiyoshauriwa kuyafanya wakati huu.  Hata utumiaji wa baadhi ya dawa kwa ajili ya maradhi yoyote uliyonayo yanapaswa kuwa na kibali cha daktari.
Vipimo vya jumla.  Ili kupunguza uwezekano wa mtoto kuzaliwa na matatizo, daktari anaweza akashauri vipimo kadhaa ili kujiridhisha.  Vipo vipimo vingi kama vile; damu, mpangilio na ubora wa seli au DNA.
Inashauriwa, unapotaka kushika ujauzito kwenye umri huo, ni vyema kufahamu hatari zilizopo na kuchukua tahadhari za kiafya kwa ajili yako na mtoto.


This post first appeared on Afya Na Kiasi, please read the originial post: here

Share the post

UNAHITAJI UMAKINI ZAIDI UNAPOKUWA MJAMZITO KUANZIA MIAKA 35

×

Subscribe to Afya Na Kiasi

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×