Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Makonda Atoa Mashitaka Kwa Rais Magufuli kwa Wanaoingia Dar na Kutoa Matamko ya Kichochezi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam amewashtaki Kwa Rais Magufuli baadhi ya watu (hajawataja kwa majina) kwa kudai kuwa wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi.

Mh. Makonda amewasilisha mashtaka hayo kwa Rais leo wakati alipokuwa akiweka jiwe la msingi la ujenzi mradi wa kuongozea ndege katika vituo vinne hapa nchini.

Mh. Makonda amemuambia Rais Magufuli kwamba kuna watu wanaingia ndani ya mkoa wa Dar es salaam na kutangaza uchochezi hivyo yeye kama kiongozi wa mkoa wanajaribu kuangalia utaratibu mzuri wa kisheria watolee matamko katika mikoa yao.

Aidha amesema kwamba "Mh. Rais Tumesikia sikia huko kwingine ila sisi kwetu hakuna waraka. Hakuna waraka popote pale ulipopita. Watu wamemwabudu bwana na mwokozi wao na Tumeungama dhambi zetu kupitia kufa kwake msalabani, tumefufuka naye na tunaendelea kufanya kazi kikamilifu".

Mbali na hayo Mku huyo wa Mkoa ameweka wazi kwamba wakazi wa Mkoa wa Dar es salaam wamesherehekea sikukuu ya Pasaka salama salimini kwani wananchi wametambua thamani ya amani.


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Makonda Atoa Mashitaka Kwa Rais Magufuli kwa Wanaoingia Dar na Kutoa Matamko ya Kichochezi

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×