Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Halima Mdee Kapata Dhamana kwa Bondi ya Milioni 20 na Viongozi Wengine Wapata Dhamana Leo


Mbunge wa Kawe Halima Mdee leo April 3, 2018 alifikiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuunganishwa na akina Freeman Mbowe

Mdee yeye alisomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa.

Baada ya kusomewa mashitaka hayo, Mahakama imempa Dhamana kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili watakaosaini kwa maandishi bondi ya Sh milioni 20 na kuripoti mara moja kila wiki.
Mahakama imesema haiwezi kumnyima mshtakiwa dhamana kwa sababu aliruka dhamana ya polisi maana polisi ni taasisi nyingine na mahakama ni taasisi nyingine, hivyo ikampatia dhamana mshtakiwa kwa masharti tajwa hapo juu.

Viongozi wengine 6 wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Halima Mdee Kapata Dhamana kwa Bondi ya Milioni 20 na Viongozi Wengine Wapata Dhamana Leo

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×