Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Ansbert Ngurumo awaasa Wanahabari wa Tanzania kutokata tamaa

Mwandishi wa Habari mkongwe wa Tanzania, Ansbert Ngurumo aliyekimbilia uhamishoni nchini Finland kwa madai ya kutishiwa maisha na maofisa wa serikali amewataka waandishi wa habari na wanaharakati nchini humo kutorudi nyuma katika kupigania uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu.

Mwandishi huyo amesambaza andiko kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii akieleza kuwa amelazimika kuondoka nchini Tanzania kutokana na kuwepo kwa mipango ya kuangamiza maisha yake. Kwa sasa anaishi nchini Finland alikopata hifadhi.


  • Nchi ya Marekani yatuma wajumbe kuichunguza serikali ya JPM

Akizungumza katika mahojiano na RFI Kiswahili kutoka nchini Finland, Ngurumo ambaye alipata kuandikia na kuwa mhariri wa magazeti ya Tanzania Daima na Mwanahalisi amekiri licha ya kutokuwepo Tanzania ataendelea kuandika mambo yanayohusu nchi hiyo.

“Ingawa sipo huko, najua kinachoendelea Tanzania na nitaendelea kuandika kuhusu nchi yangu, kinachonifanya niwe hapa (Finland), nataka kuwa hai. Ninawaomba,”amefahamisha na kuwaasa waandishi wa habari kujihadhari.

Kuhusu uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania, Ngurumo amesema haupo tena akitolea mfano wa habari zinazoandikwa na magazeti na zinazotangazwa na redio na luninga.



“Kuna masuala mengi ya msingi yanayopaswa kuhojiwa lakini yanafia chini kutokana na mazingira yalipo Tanzania. Woga umetawala katika vyombo vingi vya habari, wahariri na wamiliki.

RFI Kiswahili imemtafuta Mkurugenzi wa idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali ya Tanzania Dr. Hassan Abbas ambaye alisema serikali ya Tanzania haina kauli juu ya suala hilo.

Credit: RFI Kiswahili


This post first appeared on Maisha Yetu, please read the originial post: here

Share the post

Ansbert Ngurumo awaasa Wanahabari wa Tanzania kutokata tamaa

×

Subscribe to Maisha Yetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×