Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

CHELSEA MDOMONI KWA BARCA AU PSG SOMA HAPA UJUE KWA UNDANI!!

Chelsea imetoka sare ya 1-1 na Atletico Madrid kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa wa kundi C, matokeo yanayoitupa nje miamba hiyo ya Hispania.


Chelsea inamaliza hatua ya makundi kwa kushika nafasi ya pili ikiwa na pointi 11 sawa na Roma ya Italia iliyokaa kileleni kwa faida ya wastani wa magoli.


Atletico ilipata bao la kuongoza dakika ya 56 mfungaji akiwa ni Saul Niguez lakini goli la kujifunga la Stefan Savic dakika ya 76, likaipatia pointi moja Chelsea.


Kuna uwezekano mkubwa sana wa Chelsea kukutana na Paris Saint-Germain, Barcelona au Besiktas kwenye hatua ya mtoano ya 16 Bora.


MATOKEO YA MECHI ZOTE ZA JUMANNE:

Kundi A:

Benfica 0 - 2 Basel

Manchester United 2 - 1 CSKA Moscow

Zilizopenya 16 bora ni Manchester United na Basel

Kundi B:

Bayern Munich 3 - 1 Paris Saint Germain

Celtic 0 - 1 Anderlecht

Zilizopenya 16 bora ni PSG na Bayern Munich

Kundi C:

 Chelsea 1 - 1 Atletico Madrid

Roma 1 - 0 Qarabag FK

Zilizopenya 16 bora Roma na Chelsea

Kundi D:

Barcelona 2 - 0 Sporting CP

Olympiacos 0 - 2 Juventus
Zilizopenya 16 bora ni Barcelona na Juventus


This post first appeared on Tanzania Hot News, please read the originial post: here

Share the post

CHELSEA MDOMONI KWA BARCA AU PSG SOMA HAPA UJUE KWA UNDANI!!

×

Subscribe to Tanzania Hot News

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×