Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi ametoa tahadhari za mwelekeo wa msimu wa mvua

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi Ametoa Tahadhari tano za mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka huu kutokana na mvua chache zinazotarajiwa kunyesha Katika Maeneo Mengi nchini.

Akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake jijini hapa ,Dk Kijazi alisema vipindi vigumu vinatarajiwa kusababisha uvyevu unyevu mdogo hatua itakayoathiri ustawi wa mazao ya kilimo, mito na mabwawa kupungua maji yake kutoka hali iliyopo kwa sasa na mlipuko wa magonjwa kutokana na uhaba wa maji.

“Athari nyingine ni mafuriko yatakayojitokeza kupitia mvua kubwa zitakazotokea kwenye maeneo yasiyokuwa na uoto mwingi,

pia kutakuwa na uhaba wa malisho ya mifugo ya wanyama katika maeneo mengi, hatua hiyo ya kupungua kwa mvua inatokana na kupungua kwa joto katika maeneo ya Bahari ya Pasifiki,”alisema.



This post first appeared on Mutalemwa, please read the originial post: here

Share the post

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi ametoa tahadhari za mwelekeo wa msimu wa mvua

×

Subscribe to Mutalemwa

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×