Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Joseph Kabila amezungumza atakavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akishukuriwa na  Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kinyago toka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea zawadi ya kinyago toka kwa Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akielekea kwenye ukumbi wa mkutano na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)  Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ujumbe wake katika mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam leo Septemba 4, 2016

mediaRais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Oktoba mwaka jana katika mji wa Beni.© AFP PHOTO/ALAIN WANDIMOYI

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo,uchaguzi unaweza kuahirishwa, ametangaza Rais Joseph Kabila wakati wa ziara yake nchini Tanzania Jumanne hii. Taarifa ambayo inaweza kuchambuliwa kutoka kila pembe katika mazingira tata ya kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.

“Uchaguzi utafanyika mwaka huu au siku nyingine.” Rais anayemaliza muda wake Joseph Kabila Kabange ametangaza kwa kwa Kiswahili kwa vyombo vya habari wakati ambapo akiendelea na ziara yake nchini Tanzania. Ameongeza kuwa ‘yote yatategemea mazungumzo yanayoendelea mjini Kinshasa.’

Joseph Kabila amesema ‘itakua bora kuandaa nchi kwa muda muafaka’, akibaini hasa kwamba wapiga kura hadi milioni kumi hawajajiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na wanaweza kujihusisha na vurugu kama watakua hawakushiriki uchaguzi.

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amepuuzilia mbali madai ya kuepo mvutano wa kisiasa nchini mwake.

Hata hivyo Rais Kabila amevinyooshea kidole cha lawama vyombo vya habari akisema vinapotosha halisi iliyopo nchini humo.

Tume ya uchaguzi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, CENI, mwishoni mwa juma lililopita, ilisema inapanga kuomba kusogezwa mbele kwa tarehe ya uchaguzi mkuu wa rais na wabunge, uliokuwa umepangwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu, sasa ufanyike mwenzi November mwaka 2018.

Tangazo la tume ya uchaguzi nchini DRC, limekuja wakati huu upinzani nchini humo ukihofia kuwa huenda rais Joseph Kabila akasalia madarakani wakati muda wake utakua umemalizika ifikapo mwezi Desemba.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini humo, Corneile Naanga, amesema kuwa wameomba uchaguzi huo usogezwe mbele ili kutoa nafasi ya kufanyika kwa maandalizi mazuri zaidi yatakayopelekea kuwa na uchaguzi ulio huru na haki.

Hivi karibuni zaidi ya watu 50 waliripotiwa kuuawa na polisi kutokana na maandamano ya upinzani dhidi ya rais Kabila.

Hayo yanajiri wakati ambapo Ufaransa, kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje Jean-Marc Ayrault, kwenye runinga ya TV5 Monde Jumatatu wiki hii, alimtaka Rais wa sasa wa DR Congo kuheshimu Katiba na kutowania muhula mwengine.

Wakati huo huo Ufaransa imetishia kuichukulia vikwazo nchi hiyo. Bw Ayrault amesema:”Rais Kabila lazima aonyeshe mfano mwema. Ni lazima aheshimu katiba. Iwapo vikwazo vitahitajika tutaamua kuvitekeleza. Nataka watu waelewe; Watu waliopo katika mamlaka DRC ni lazima wawajibike. Iwapo wanahitaji amani nchini mwao, iwapo wanajali hali ya watu wao ,ni lazima wafuate katiba”.

Seerikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kwa upande wake, imesema Ufaransa inachochea maasi dhidi ya serikali nchini humo.

Waziri wa Mawasiliano Lambert Mende ameliambia shirika la habari la AFP kwamba Ufaransa ‘inacheza mchezo hatari’

The post Joseph Kabila amezungumza atakavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania appeared first on KIVUMEDIA.This post first appeared on KIVU MEDIA – La Voix De Kivusien, please read the originial post: here

Share the post

Joseph Kabila amezungumza atakavyoshirikiana na Serikali ya Tanzania

×

Subscribe to Kivu Media – La Voix De Kivusien

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×