Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Sekondari

Mkazi wa Manzese, Dar es Salaam, Amiri Shekhe (25), amepandishwa kizimbani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni  kwa tuhuma za Kumpa Mimba Mwanafunzi wa kidato cha tatu.

Akimsomea mashtaka jana mbele ya Hakimu Anifa Mwingira, Mwendesha Mashtaka wa Serikali, Hilda Kato alidai kuwa Novemba 10, mwaka huu eneo la Mvuleni Manzese wilayani Ubungo, mshatakiwa alimpa Mimba Mwanafunzi wa kidato cha tatu mwenye umri wa miaka wa 17.

Mshtakiwa alikana kutenda kosa hilo na Kato alisema upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba mahakama ipange tarehe nyingine.

Hakimu Mwingira alisema dhamana ipo wazi kwa mshtakiwa kwa kutakiwa Kutimiza Masharti ya kuwa na wadhamini wawili ambao kila mmoja atasaini bondi ya Sh 500,000.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana na kurudishwa rumande hadi Agosti 19, mwaka huu kesi hiyo itakapokuja kutajwa tena.
This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

Afikishwa Mahakamani Kwa Kumpa Mimba Mwanafunzi wa Sekondari

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×