Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Mwanamke Auawa Katika Harakati za Kutaka Kubakwa

Regina Manday (35), aliyekuwa anafanya kazi kwenye shamba la mwekezaji Rift Wall Plantation Kijiji Cha Magara Halmashauri ya Babati, ameuawa Katika Harakati za kubakwa.

Taarifa ya mama huyo kuuawa ilitolewa mwishoni mwa wiki na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Augustino Senga, na kusema tukio hilo lilitokea Aprili 15, mwaka huu saa 1:00 usiku,  baada ya kupigwa mweleka na kuanguka chini.

Kamanda Senga alimtaja mtuhumiwa wa mauaji hayo ni Claud Swedi maarufu kama Claud Safari (35), mkulima na Mkazi wa Kijiji cha Moya, na amekamatwa.

“Chanzo cha mauaji haya marehemu alikuwa anakwenda kulala kambini kutokana na kufanyakazi za kibarua… wakati anapita maeneo ya korongoni kwenye  mto, ndipo alipigwa mtama na kuangukia kisogo na kufariki dunia,” alisema Senga.
This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

Mwanamke Auawa Katika Harakati za Kutaka Kubakwa

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×