Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

HIZI HAPA SHULE 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018,MWANAFUNZI BORA...TUMAINI LUTHERAN IMEFUTIWA MATOKEO

Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya Kidato Cha Nne mwaka 2018, na kutaja shule 10 zilizofanya vyema katika mtihani huo kwa shule zenye watahiniwa zaidi ya 40.Wakati shule binafsi zikifanya vyema, mwanafunzi aliyefanya vizuri zaidi katika mtihani huo ni wa shule ya sekondari Ilboru ya Arusha, Hope Mwaibanje.

Akitangaza matokeo hayo leo Alhamisi Januari 24, 2019 mkoani Dodoma katibu mkuu wa baraza hilo, Dk Charles Msonde amezitaja shule hizo kuwa ni St Francis Girls (Mbeya), Kemebos (Kagera), Marian Boys, Ahmes, Marian Girls (zote Pwani), Canossa, Bright Future Girls (zote Dar es Salaam), Maua Seminari (Kilimanjaro), Precious Blood (Arusha) na Bethel Sabs Girls (Iringa).

Katika matokeo hayo, watahiniwa 252 wamefutiwa matokeo kutokana na udanganyifu na kati yao, 71 ni wa kujitegemea huku wawili kati yao wakiandika matusi.

Wakati huo huo (Necta) imefuta matokeo ya wanafunzi 57 wa Kidato Cha nne katika shule ya Sekondari ya Tumaini Lutheran Seminari ya Malinyi mkoani Morogoro baada ya kubaini shule hiyo kuvujisha mtihani huo.


Mbali na kufuta matokeo hayo, Necta imekifungia kituo hicho cha kufanyia mtihani.

Hayo yameelezwa leo Alhamisi Januari 24, 2019 na Katibu Mkuu mtendaji wa baraza hilo, Dk Charles Msonde wakati akitangaza matokeo ya kidato Cha Nne mwaka 2018 mkoani Dodoma.

Amesema wameagiza wahusika wote kuchukuliwa hatua wakiwemo polisi waliosimamia.


This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

HIZI HAPA SHULE 10 BORA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2018,MWANAFUNZI BORA...TUMAINI LUTHERAN IMEFUTIWA MATOKEO

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×