Get Even More Visitors To Your Blog, Upgrade To A Business Listing >>

Wafanyabiashara Morogoro watelekeza masoko yao na kuhamia katikati ya mji.

Siku chache baada ya Rais Dokta John Pombe Magufuli kuwataka wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya zote nchini kuacha kuwabughudhi wamachinga na badala yake wawatafutie maeneo maalumu ya kufanyia biashara zao hali imekuwa tofauti kwa Manispaa ya Morogoro baada ya Wafanyabiashara mbalimbali kuyatelekeza masoko na kupeleka bidhaa zao katikati ya mji huku wafanyabiashara wa maduka wakilalamikia Maduka yao kuzibwa na bidhaa hizo.
Wakizungumza na ITV wafanyabiashara hao wa maduka wametupia lawama uongozi wa wilaya kushindwa kusimamia agizo la Rais kwani wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa chini na kuziba maduka sio wale aliowalenga Mheshimiwa Rais Magufuli.

ITV imeshuhudia meza na vikazi vikiwa wazi katika soko kuu la Manispaa la Manzese walikohamishiwa wafanyabiashara wote huku waliobaki nao wakiazimia kulitelekeza soko hilo na kufuata wateja maeneo ya mjinikushinikiza waliotoroka kurejeshwa sokoni hapo.

Kufuatia malalamiko hayo mkuu wa wilaya Morogoro Bi.Regina Chonjo amesema serikali haitawavumilia wafanyabiashara walionukuu vibaya kauli ya Rais na badala yake halmashauri inapanga utaratibu wa kuhakikisha wale wote waliotoroka katika maeneo yao ya biashara na kuwa kero kwa wengine wanarudishwa mara moja.

chanzo: Itv


This post first appeared on MASWAYETU, please read the originial post: here

Share the post

Wafanyabiashara Morogoro watelekeza masoko yao na kuhamia katikati ya mji.

×

Subscribe to Maswayetu

Get updates delivered right to your inbox!

Thank you for your subscription

×